Nisaidieni ndugu zangu, ungekua na rafiki kama huyu ungefanyaje!

Kwa mtazamo wangu huyo rafiki yako anataka mgombane na mpenzi wako halafu yeye ndio ashike usukani achana na rafiki huyo
 
Anataka mgombane amchukue yeye na ukichunguza vizuri kuna uwezekano anakusema vibaya kwa binti pia.
 
Achana na rafiki yako. Akikuambia mwambie unajua. Na pia mueleze msichana wako. Lazima utakuta jmaa kamtongoza
 
Poleni na pilika za hapa na pale,

Nimekua na uhusiano na binti takribani mwezi wa tano sasa niko nae,
Sasa wakuu nina rafiki yangu naishi nae jirani yaani tumepanga nyumba karibu karibu,
Vilevile huyu rafiki yangu ninafanya nae kazi kwenye kampuni moja,

Kilichonifanya nije kuonba ushauri kwenu ni kwamba huyu rafiki yangu anafatilia sana mienendo ya mpenzi wangu na kuja kuniambia, mbaya zaidi anafatilia mambo yake mabaya tu ndio anakuja kuniekeza,
Kila akimuona kasimama na mwanaume taarifa lazima aniletee,
Akimkuta barabarani anatembea na mwanaume utashangaa nishatumiwa text ooh mpenzi wako yuko na wanaume hapa sehemu fulani,
Kuna siku aliniambia eti demu wako hajatulia maana ni mzurulaji sana huwa nakutana nae mataani sana

Juzi kati nilimwambia mpenzi wangu kaenda kwenye mkutano somewhere, jamaa kaniambia eti wanawake ni waongo sana itakua ameenda kugongwa sehemu fulani,

Sasa leo asubuhi tulikua tunaongea kuhusu ishu za kupigwa mzinga na mademu, nikamwambia mimi mpenzi wangu hanipigagi mzinga waga hata kumpa hela wakati mwingine nampatia mwenyewe hata hajaniomba au hata akiniomba huniomba kwa ustaarabu,
Jamaa akanijibu eti huyo itakua kuna lijamaa linamgonga kwaiyo linamuhonga pesa nyingi"

sasa leo nilikua kazini mida ya jioni nikaona text imetoka kwa huyo rafiki yangu
Jamaa kanitumia text eti "yani huyu demu wako hapa hauna demu kabisa"
Nilipomuuliza kwanini akajibu eti yaani nimekutana nae njiani anaongea na simu anamdirect jamaa eti waonane"

Kiukweli mi nimekosa hata cha kumjibu wakuu nimelileta kwenu mimi nifanyeje?
Ungekua wewe ndiyo una rafiki wa hivi ungefanyaje?

Msichana mwenyewe bado sijamueleza chochote
Cha kwanza huyo sio rafiki ni mshkaji. Rafiki huwa kuna vigezo na huyo hana hata kimoja. Mchane tu mshkaji mwambie huwezi kutoka na yeye. Mahusiano yako hayamhusu hata punje so apite kushoto.
 
Mi huwa nawashangaa sana wanaume ambao nakuwa hajui chochote kuhusu mpenzi wake.

Kabla sijaletewa taarifa yeyote na mtu yeyote mimi mwenyewe nakuwa najua anaongeaga na nani kwenye simu yake, ratiba zake zote bila yeye kujua. So hata mtu ainiletea taarifa yeyte anakuwa anapoteza mda tu.
 
Pilipili Asiyoila yamwashia nini... tell him to find something better to do.... habari za demu wako aachane nazo hazimuhusu
 
Kwahyo umekuja kunireport humu au siyo,hamna noma man nitaacha kukupa hizo taarifa isiwe kesi......
 
Nilishakuwa na situation kama hii
Nilikuwa na rafiki yangu wa kiume ananiletea mabaya tu ya my man,mbaya zaidi sikuwa na namna yoyote ya kuprove kama ni kweli ama uongo sababu sina muda na sipendi kufatilia mtu yoyote
Kimsingi nilichojifunza ni kuweka mahusiano/maisha yako yawe yako peke yako...usiruhusu mtu wa nje aingilie kwa namna yoyote,kama ni kweli huyo mwanamke wako ana mabaya anayofanya niamini utayagundua soon or later
Huyo rafiki yako unaweza kumkataza tu aache kuingilia maisha yako
Wewe na Joseverest waga mna undugu eeh??
 
Akishikwa na ashki
Nani anakupunguzia uzito kati ya rafiki yako na demu wako ?
 
Nimewahi kuwa kwenye situation kama yako, tofauti ni kwamba Mimi jamaa hakua close friend. Baada ya kufanya uchunguzi Nikagundua jamaa alikua anamtaka na in kweli demu alikua kicheche.
 
Back
Top Bottom