Umemaliza mkuu.Hapa kuna mambo 3 tu moja huenda jamaa alishataka mzigo kabla ako akakosa mbili huenda jamaa anamta ale mzigo tatu au jamaa anataka umuoe yeye
Cha kwanza huyo sio rafiki ni mshkaji. Rafiki huwa kuna vigezo na huyo hana hata kimoja. Mchane tu mshkaji mwambie huwezi kutoka na yeye. Mahusiano yako hayamhusu hata punje so apite kushoto.Poleni na pilika za hapa na pale,
Nimekua na uhusiano na binti takribani mwezi wa tano sasa niko nae,
Sasa wakuu nina rafiki yangu naishi nae jirani yaani tumepanga nyumba karibu karibu,
Vilevile huyu rafiki yangu ninafanya nae kazi kwenye kampuni moja,
Kilichonifanya nije kuonba ushauri kwenu ni kwamba huyu rafiki yangu anafatilia sana mienendo ya mpenzi wangu na kuja kuniambia, mbaya zaidi anafatilia mambo yake mabaya tu ndio anakuja kuniekeza,
Kila akimuona kasimama na mwanaume taarifa lazima aniletee,
Akimkuta barabarani anatembea na mwanaume utashangaa nishatumiwa text ooh mpenzi wako yuko na wanaume hapa sehemu fulani,
Kuna siku aliniambia eti demu wako hajatulia maana ni mzurulaji sana huwa nakutana nae mataani sana
Juzi kati nilimwambia mpenzi wangu kaenda kwenye mkutano somewhere, jamaa kaniambia eti wanawake ni waongo sana itakua ameenda kugongwa sehemu fulani,
Sasa leo asubuhi tulikua tunaongea kuhusu ishu za kupigwa mzinga na mademu, nikamwambia mimi mpenzi wangu hanipigagi mzinga waga hata kumpa hela wakati mwingine nampatia mwenyewe hata hajaniomba au hata akiniomba huniomba kwa ustaarabu,
Jamaa akanijibu eti huyo itakua kuna lijamaa linamgonga kwaiyo linamuhonga pesa nyingi"
sasa leo nilikua kazini mida ya jioni nikaona text imetoka kwa huyo rafiki yangu
Jamaa kanitumia text eti "yani huyu demu wako hapa hauna demu kabisa"
Nilipomuuliza kwanini akajibu eti yaani nimekutana nae njiani anaongea na simu anamdirect jamaa eti waonane"
Kiukweli mi nimekosa hata cha kumjibu wakuu nimelileta kwenu mimi nifanyeje?
Ungekua wewe ndiyo una rafiki wa hivi ungefanyaje?
Msichana mwenyewe bado sijamueleza chochote
Wewe na Joseverest waga mna undugu eeh??Nilishakuwa na situation kama hii
Nilikuwa na rafiki yangu wa kiume ananiletea mabaya tu ya my man,mbaya zaidi sikuwa na namna yoyote ya kuprove kama ni kweli ama uongo sababu sina muda na sipendi kufatilia mtu yoyote
Kimsingi nilichojifunza ni kuweka mahusiano/maisha yako yawe yako peke yako...usiruhusu mtu wa nje aingilie kwa namna yoyote,kama ni kweli huyo mwanamke wako ana mabaya anayofanya niamini utayagundua soon or later
Huyo rafiki yako unaweza kumkataza tu aache kuingilia maisha yako
Hatuna unduguWewe na Joseverest waga mna undugu eeh??