Nisaidieni kwa Hili Ndugu Zangu

Nisaidieni kwa Hili Ndugu Zangu

Bobuk

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
5,870
Reaction score
3,275
Nakumbuka kuna wakati serikali ilitoa amri kwamba watumishi wote wa serikali lazima wapate japo elimu ya kidato cha nne, na wapate cheti ili kuthibitisha hiyo elimu yao. Wale wote ambao walikuwa wameruka au wamekosa kuipitia hatua hiyo kwa sababu moja ama nyingine walipewa muda maalum wa kufanya hivyo. Maamuzi ya awali ilikuwa kwamba wale ambao muda huo utapita wakiwa hawajatekeleza masharti ya amri hiyo watakuwa wamefukuzwa kazi, ila baadaye masharti yakalegezwa kwamba hawataweza kupandishwa madaraja kutoka pale walipo. Sina taarifa kama ndivyo ilivyokuwa au yalikuwa maneno tu, wahusika na watawala wa ofisi za serikali wanajua.

Kutokana na amri hiyo watu walijikita kwenye masomo. Wahudumu/wasaidizi maofisini, wahazili, madereva na wengineo wote walilazimika 'kuingia msituni' kukwepa rungu hilo. Sina hakika kama kuna uwezekano wa mtu kupata ajira kwenye ofisi hizo bila hiyo elimu kwa sasa.

Sasa hili suala la kusema mbunge hatakiwi kuwa na angalau elimu fulani linanitatiza sana. Yaani tunamwekea masharti ya kusoma miaka minne ya sekondari atakayekuwa anafanya usafi ofisini kwa kudaii ni sharti la lazima na muhimu, lakini tumesema hilo halina umuhimu kwa mbunge ambaye ninaamini anatakiwa awe na majukumu makubwa sana kuliko anayefanya usafi ofisini. Yeye mbunge tumesema anatakiwa ajue tu kusoma na kuandika jina lake (ili wakati wa kuchukua posho asije akashindwa kusoma vizuri jina lake na kujikuta akitia saini kwenye jina la mheshimiwa mwenzake akamsababishia usumbufu usiokuwa wa lazima)!

Huyu anahusika katika kutunga na kurekebisha sheria za nchi, kusimamia idara nyeti za serikali kupitia kamati za bunge, kuisimamia na kuiwajibisha serikali katika utendaji wake wa kila siku. Huyu anayo mamlaka ya kuwawajibisha watendaji wa serikali kama mawaziri, waziri mkuu hata Rais inapobidi. Huyu ni mwakilishi wa wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo katika maeneo yao. Na zaidi ya hayo tunamlipa mamilioni kwa mwezi kama mshahara na posho (siyo kama yule mhudumu wa ofisini anayeambulia kima cha chini tu).

Pamoja na sifa zake zote na wajibu wake huo, tumesema elimu si muhimu kwake kama mfagiaji wa ofisi. mfagiaji wa ofisini anatakiwa kwanza ajue kiingereza kwa sababu vumbi la ofisini limetoka kwenye viatu vya wasomi, usipolifagia 'kiingereza' au 'kisomi-somi' haliondoki! Hata dereva wa gari la serikali asipoingiza gia kwa mkono uliofanya mtihani wa NECTA zitakuwa zinagoma kila wakati hivyo kuhatarisha maisha ya maafisa na mali za serikali.

Ila kwa mbunge kwa sababu kazi yake ni kuongea tu, bila kujali kama anachoongea ni cha kweli au la, mradi ameongea hakuna sababu ya mtu huyu kuhangaika na elimu. Kwanza hata asipoongea, akiweza kulala mwanzo na kuamka mwisho wa kikao hakuna tatizo, mradi tu asishindwe kuona jina lake wakati wa kutia saini!

Mambo mengine yanashangaza sana, hadi kufikia hatua unashindwa kuyashangaa. Lakini tutafika tu. hata mkuu wa boma alisema siku moja kuwa 'ndio hao hao tulio nao'...tutafika tu
 
Kwanza mimi mbuge wangu ni darasa la saba na wengi wengi pale ccm ndiyo maana,walifanya hivyo ili kuepuka mpasuko,wao ni maslahi tu....
 
Je wajua kwamba, elimu ya chini ili kuwa dereva serikalini Tanzania ni KIDATO CHA NNE huku elimu ya chini ili kuwa mbunge Tanzania NI KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA?
 
Dereva anayeendesha magari ya serikali anatakiwa awe na elimu ya kidato cha nne na cheti kutoka VETA au N.I.T lakini mbunge wake anayetunga sheria anatakiwa kujua kusoma na kuandika tuu...siitaki hii katiba
 
Kwa kawaids wabunge wanakuwa na study tours kwenye nchi mbalimbali
Sasa kweli hawa KKK wataelewa kinachozingumzwa? F4 ingekuwa kipimo sahihi. Hata wakati wa kuchambua hoja inahitajika uelewa wa aina fulani wa mada. Hivi kweli tunaenda wapi? Hii itawavunja moyo wanaopenda kusoma. Halafu bahati mbaya waliopitisha hii kitu wengi wao ni shahada ya kwanza hadi maprofesa. Hii ngumu kumeza.
 
Hahahahaaaa tanzania ni zaidi ya uijuavyoo
 
Dereva anayeendesha magari ya serikali anatakiwa awe na elimu ya kidato cha nne na cheti kutoka VETA au N.I.T lakini mbunge wake anayetunga sheria anatakiwa kujua kusoma na kuandika tuu...siitaki hii katiba

Na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ni mtu aliyefeli kidato cha sita.
 
Kwa kawaids wabunge wanakuwa na study tours kwenye nchi mbalimbali
Sasa kweli hawa KKK wataelewa kinachozingumzwa? F4 ingekuwa kipimo sahihi. Hata wakati wa kuchambua hoja inahitajika uelewa wa aina fulani wa mada. Hivi kweli tunaenda wapi? Hii itawavunja moyo wanaopenda kusoma. Halafu bahati mbaya waliopitisha hii kitu wengi wao ni shahada ya kwanza hadi maprofesa. Hii ngumu kumeza.

Hivi kukiwa na wabunge waelewa unadhani ile mikataba feki itapenya? Hiyo ndiyo sababu kubwa kaka.
 

Yeye mbunge tumesema anatakiwa ajue tu kusoma na kuandika jina lake (ili wakati wa kuchukua posho asije akashindwa kusoma vizuri jina lake na kujikuta akitia saini kwenye jina la mheshimiwa mwenzake akamsababishia usumbufu usiokuwa wa lazima)!
nchi hii inaendeshwa kichwa chini miguu juu.
lakini hata wananchi nao hawanazo. wanajua kabisa huyu ni mbumbumbumbumbu..... lakini bado wanamchagua.
ndivyo tulivyo.
 
Kwa maoni yangu hata elimu ya kidato cha nne kwa nafasi ya ubunge bado ni ndogo kwa ulimwengu wa leo, na mbaya zaidi wameondoa kile kipengere cha waziri asiwe mbunge, maana yake huyu mbunge wa KKK anaweza kuwa waziri!
 
Back
Top Bottom