Nisaidieni Kuisaidia Tanzania!


Dijovisonjn

Dijovisonjn

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Messages
462
Likes
2
Points
35
Dijovisonjn

Dijovisonjn

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2011
462 2 35
Binafsi huwa siamini katika kulalamika, siku zote nimekuwa mfuasi mzuri sana wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayonizunguka!

-Tanzania ni maskini.
-Tanzania ujinga. umeongezeka.
-Tanzania maradhi ni mengi.
-Tanzania ina mfumo mbovu wa kiutawala. n.k

Matatizo haya yote niliwahi kuyatafakari na kujaribu kuweka assumptions mbalimbali zinazotolewa na watu mbalimbali lakini sikuwahi kupata majibu ya moja kwa moja ya kutatua haya matatizo ya Tanzania, baadhi ya hizo assumptions ni kama vile:
a) KUBADILI MFUMO WA KIUTAWALA, hapa najiulza ni mfumo gani bora utakaotufaa watanzania? Parliamentalism au Presidentalism? (kumbuka semi presidential tulionao sasa umefail) au tutoke kabisa kwny mfumo wa kidemokrasia na tuingie kwenye udikteta?

b) 2015 KUITOSA CCM NA KUICHAGUA CHADEMA, Binafsi sijawahi kupata jibu la moja kwa moja ni kvp CHADEMA inaweza kuifanya Tanzania nchi ya neema? Je ni kwa kuwapeleka mafisadi mahakaman? Au kuanzisha system ya uwajibikaji kwa viongozi? Au kwa kuendelea na ''peoples power yao? (kvp wakat wao ndio watakuwa madarakan?)

c) KUPUNGUZA MADARAKA YA RAISI, hapa mi nadhan hata tukiamua kumfanya raisi ceremonial leader kama alvyo malikia wa U.K au raisi wa German, cdhan kama itasaidia kutukomboa katika matatzo tuliyonayo.

d) KUWA NA TUME HURU YA UCHAGUZI, naamin kwamba kuwa na tume huru ya uchaguz bado haitosaidia kututoa kwenye matatizo yetu zaidi tu ya kujitengenezea CV (kama waliyonayo Ghana) ya kuwa nchi ya kwanza au ya pili au ya tatu barani Afrika kuwa na uchaguzi huru na wa haki zaidi na hilo sioni jipya lolote.

My take: kusudio langu ni kuomba msaada wa mawazo yako ili yanisaidie wakati nitakapokuwa natoa maoni yangu juu ya katiba mpya nitoe maoni yatakayoisaidia Tanzania na watanzania katika kutatua matatizo yao (yetu) yanayotukabili na nisitoe mawazo kwa ajili ya ushabiki wangu wa kisiasa nilionao/nitakaokuwa nao.
 

Forum statistics

Threads 1,274,223
Members 490,631
Posts 30,505,197