Jenerali QoyoJB
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 304
- 163
Sio upofu
Dada yako kajitoa fahamu
Na anataka watu wacheze kwaito....
Heheheheh
Unatumika na wewe unafumba macho
Kama unaona umri unakimbia kubali akuoe ili uhudumie mkewe na wanae
asante sana kwa ushauri lakini mimi na yeye hatujakutana kwenye mtandao wowote tulikutana wenyewe tuu tukazoeana na ikafikia mpaka hapo. asante
Dada achana na huyo mtu muda uliopoteza siyo mwingi kuliko matatizo unayokaribisha kwenye maisha kwa muda mrefu wa maisha yako. Kwanza ni muongo na anakutumia kama kitega uchumi cha kulea watoto wake. Amekwambia watoto wawili kumbe wanne? Sasa wewe utazaa wangapi jumla wawe wangapi na mtalea vipi? Atakutia presha siku ukigundua mengine. Hadi hapo mshukuru Mungu amekufungua macho sasa ukiendelea usimlilie Mungu tena maana utakuwa umekaidi mwenyewe. Kama unaendelea naye endelea kama starehe yako tu usikose dushelele ghafla ila angalia utaratibu mwingine. Kwa umri wako bado unapata mume fresh tena una kazi yako unahofia nini? Jambo la pili nakutahadharisha ni kuhusu uraia. Huyo ni mkenya wewe ni mtanzania je uko tayari kubadili uraia wako kwasababu tu ya kuwa mke wa pili? Je siku ukihamia kenya maisha yatakuwaje na huyo bi mkubwa? Unajua hao watoto wake wanaopata shida na mama yao wanakuona wewe ndo unakula hela za baba yao hivyo wataku treat kama malaya siku wakipata nguvu utajuta kumfahamu huyo mkenya. Kama hajakutia mimba tafuta njia ya kuchomoka. Suala la tatu kwamba huyo mtu hafai ni hiyo unasema ana wasichana wengine kibao anawapeleka hadi kwake siku haupo. Sasa hapo dadangu bado hujiongezi? We kwa huyo mtu ni mchepuko tu kama michepuko mingine wala siyo mke mtarajiwa! Najua sikio la kufa halisikii dawa! Ila uamuzi ni wako sisi tunaishia kushauri kama ulivyoomba.
pachambili, huyo sio mume ila anakutumia wewe kuweka unafuu ktk familia yake, ni afadhal sana maumivu utakayopata sasa baada ya kumuacha kulikon yajayo baada ya kuolewa, na anasisitiza maana kuhusu ndoa mbili coz kwako anauhakika na hela, ila blieve me unatumika mama, relax utampata amua leo na utulie, wako anakuja huyo wa watu
pole sana naamini umejifunza kitu......achana nae jipange upya
Samahani # naomba uniruhusu kucheka and then nisinzie! Thank u jf
Hahahahaa! Hata niwe na miaka 1000000 sifugi mwanaume
Hakuna mapenzi hapo huyo ni mnafiki anataka atumie pesa! Zako.ni kicheche kama vicheche wengine piga chini fasta.muda unao wa kukaa na kumwomba mungu atakupa mume wako..wakenya ni vichecheyuko kimaslah zaidi. Usiogope kuhusu kufahamika kwake kwa wazaz wako,fikiria maisha yako jua unataka kujiingiza kwenye matatizo ya kumlelea familia..uzuri na raha ya mwanamke utunzwe kama malkia na siyo kuumiza akili etifamilia kesho itakula nin, cjui ada nitapata lini looo. .mwanamke unatakiwauwaze mastayle ya mapenz na jinsi ya kumnyenyekea mumeo. ..asikuzeeshe bure na mawazo. .mwambie kama vipi apite vileeee akuondolee uchuro hapa. .ujana wake ale na nan na wewe uzee aje kula mturuhusu..mfyuuuuzake
asante sana tena sana yaani nimetumika sana ila kesho ni hitimisho
Pole sana, ushauri gani unaotaka hapa baada ya kudanganywa kiasi hiki!? Mwambie afungashe virago vyake haraka sana toka kwako. Asikutafute kwa namna yoyote ile.
dada pole saaana. ila mungu ndo mwenye majibu kukuoesha hayo kuna maana saaana katika maisha yako. pata muda wa kuongea na mungu kwa kumaanisha utajibiwa tu kama anafaa ama la. ila muondoe kabisa unapoomba ilg mungu akuoneshe mwenyewe apendavyo.
Haya yasiwe maneno tu hunu,vitendo ndo vitakusaidia zaidnashukuru sana nimejifunza sana tena sana na sitafeli tena mitihani kama hii, nikimwambia namuacha analia kama sinema za kihindi ila sasa hata atoe machozi aya damu ndiyo ameshanikosa
Sio upofu
Dada yako kajitoa fahamu
Na anataka watu wacheze kwaito....
Haya yasiwe maneno tu hunu,vitendo ndo vitakusaidia zaid