Nipashe, Wamama kujinunulia Vifaa vya Kujifuungulia- Ila Magufuli ananunua Ndege.

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Kazi Kubwa ya Serikali Katika Uchumi wa Soko huria sio Kufanya Biashara wala Kuchukua Fedha za Kodi kufanyia Biashara za Alinacha na Abunuwasi. Kazi Kubwa ya serikali Katika Uchumi wa soko huru, Ni kujikita zaidi na 1) Kujenga infrastructure, kama Barabrara Reli, Viwanja vya Ndege, Bandari.
2) Kuimarisha Technologia ya Mawasiliano Kama Communication Satellite, Fiber optics backbones, na Mitandao mingine ya Mawasiliano, Bila kusahau njia kuu za usambazaji wa umeme.
3)Kuimarisha elimu na Utafiti, 4) Kuimarisha Huduma za Afya.
5) Kulinda Nchi na usalama wa Raia na Kuhakikisha kunakuwepo haki, utawala wa sheria. amani na Stability.
6) Kuhakikisha Kama Taifa kuna sera ya Kuhakikisha Kuwepo na Food security.
7) Kugharimia Uendeshaji wa kila siku wa serikali, Sio kubeba bakuli, na kuomba omba pesa za kuendesha serikali nchi zingine wakati kodi zenu mnazitumia vibaya kununua ndege kutaka sifa za kijinga. Kwani wahisani wawape pesa wao wanazipata mbinguni? Si ni kodi za wananchi wao. Sikatai kusaidiwa kama nchi lakini musaidiwe pale ambapo mumeonyesha responsibility!

Kwa Kufupisha Ni Kuwa Niseme Kazi za Kwanza za Muhimu kwa Kodi za Wananchi ndizo hizo. Kama hayo mambo hapo juu unayapuuza na Unachukua fedha za Kodi tena bila kuheshimu budgeti, Unaenda Kufanyia Biashara ambayo ingefanywa na sector binafsi, Tena biashara zenyewe ni Kuchukua Pesa Keshi za Umma na kunulia Ndege ambazo zinaweza kucrush kesho, huku wamama wakinunua gloves za kuhudumiwa wakiwa katika Uzazi, Huo ni Wazimu, Wazimu wa Karne!
 
Wanawake ndio huwa wanalishabikia na kulichagua hili lichama siwezi kuwaonea huruma hata....
 
Hivyo vifaa vya kujifungulia ni utaratibu na haujaanza mwaka 2016 upo toka zamani.
 
nyie mmeshindwa tu kujenga ofisi nzuri ya chama licha ya kupata ruzuku ndeefu huku mikoani hali mbaya mpaka bendela zimewekewa viraka
 
Juzi nimempeleka shemeji yenu nikaambiwa hakuna kidonge cha aina yeyote hata panadol, Sindano nikanunue mtaani na Dawa ya kuchomea wao wanamaji ya drip tu na hiyo ni hospital ya wilaya. ......huyu uongozi wake hauna connection kabisa.....
 
Hivyo vifaa vya kujifungulia ni utaratibu na haujaanza mwaka 2016 upo toka zamani.
Umenena ukweli Ruta..huwa utaratibu ushazoeleka toka zamani. Huu wa Ndege ni mpya nao utazoeleka kama mazoea mengine. Ila kada mwenzangu hivi wazazi kujinunulia vifaa vya kuzalia imo kwenye SERA ya Afya au mazoea tu...maana Sera yasema wazazi wanapatiwa huduma buree za uzazi lakini hapa unazungumzia mazoea. Tuwasaidie kinamama maana ndio wanaotupa kura za ushindi kila mara kwa Sera zetu nzuri ambazo kwa kweli hatuzitekelezi..
 
Kweli mmekosa kick, kila anachokifanya rais lazima mkijadili na mkilalamikie, mnakoelekea, mnakaribia kuhoji hata nguo zake za ndani anazovaa ...poleni sana.
Wewe lazima umekula 10% ununuzi cash ndege pia Tenda za ujenzi wa ndege chato ni yako hata dili la Lipumba kula pesa za Umma azitumie kuua CUF na kudhoofisha ukawa umo,kwa utetezi huo lazima unanufaika na mengi toka CCM.
 
Ni Tanzania pekee MTU anabeba mimba miezi bila ya kujianda kujifungua lazima ifike mahali tubadilike hakuna kitu kinachoboa kama hivi hats hii Sera ya wizara inatakiwa ibadilishwe.. Service atapewa Bure lakini vifaa anatakiwa kununua. Mh Raising anajitahidi mnyonge mnyongeni lakin haki ya mpeni.... Mambo meng Mh kafanya ni mazuri sio kupnga kila kitu
 
Umenena ukweli Ruta..huwa utaratibu ushazoeleka toka zamani. Huu wa Ndege ni mpya nao utazoeleka kama mazoea mengine. Ila kada mwenzangu hivi wazazi kujinunulia vifaa vya kuzalia imo kwenye SERA ya Afya au mazoea tu...maana Sera yasema wazazi wanapatiwa huduma buree za uzazi lakini hapa unazungumzia mazoea. Tuwasaidie kinamama maana ndio wanaotupa kura za ushindi kila mara kwa Sera zetu nzuri ambazo kwa kweli hatuzitekelezi..
Tanzania ni Nchi tajiri sana kwani imeuduwaza Dunia kununua Ndege cash hata Oman,Waarabu wenye pesa nyingi hawanunui ndege cash,sasa uwanja unajengwa Chato kwa cash pasipo Tenda kutangazwa,mshauri wa Uchumi bwana yule Profeselii Lipumba anapiga pesa kila kona zote,pesa inayopotelea hapo ingeweza kujenga Hosptal za rufaa kila mkoa na kuwaajili madaktari toka india wagonjwa wakatibiwa hapa pasipo kuingia gharama kwenda india.
 
Back
Top Bottom