Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Kasseja na Ngassa ni watu ambao mapenzi yao kwa Club za Kkoo,yako wazi.Ngassa pamoja na kucheza Simba,inasadikika anaipenda sana Yanga hali kadhalika,Kasseja kuja yanga bado ataendelea kuipenda Simba.
Kuipenda timu sio tatizo hata kidogo,Walcott ni shabiki wa Liverpool ila anacheza arsenal na akikutananao,anawafunga magoli kama kawaida.#Stamina alisema "unaweza kuwa shabiki wa Simba na ukaishi mwembe Yanga"
Ukimuuliza Steven Mazanda wa MCC anashabikia timu gani,akisema YANGA mimi sioni tatizo au ukimuuliza Salum Kanoni wa Kagera sugar akisema yeye ni shabiki wa Simba mimi sioni tatizo pia.
Kasseja hakuongezwa mkataba na Simba si kwa sababu ya umri wala kushuka kiwango,ni siasa zinazoendesha Club ya Simba na Yanga nao,wamemsajili kwa siasa hizo hizo!!
Anyway,mashabiki wanatakiwa kuelimishwa ili wajue kwamba,unapochezea YANGA sio lazima uwe shabiki wa timu hiyo.Hivi unadhani NIYONZIMA ni shabiki wa YANGA? unadhani TAMBWE ni shabiki wa SIMBA?
ikitokea siku yanga wamepigwa 5 golini akiwa kaseja wasiseme kaachia.............!!
I'm sorry!