Anza na biashara lakini biashara inahitaji plan nzuri....
Kama unanunua kiwanja hakikisha ni sehemu ambayo mtu anauzia shida na kimekaa sehemu ambayo ukikinunua miaka kadhaa thamani yake itakuwa kubwa sana
Usigeenda kuzika hela sehemu porini halfu uka mjini kutafuta hela.
Kuna dogo alinifuata amepiga deal ya 1.3M anataka aanze kujenga kijijini kwako taratibu taratibu huku anaendelea na kazi.Nikamuuliza hiyo nyumba ikikamilika utaenda kukaa, akasema kazi ikiisha nitarud home.Nikamuuliza M1.3 nyumba itafika wapi? Akasema kwenye renta maana ni vyumba vitatu tofauli za kuchoma(tshs.100).
Nikamwambia acha uoga kabla ujawa na kazi hii ulikuwa boda boda,nunua pikipiki used mpe mtu akupe pesa hlf kila mwezi ongezea mshahara,Jenga huku pesa inaingia.Nahisi dogo alikuwa na zile akili za kijijini Mtu nyumba basi akajenga ikafika juu ya dirisha, Hela ikakata.Miezi miwili mbele bahati mbaya akafukuzwa kazi hata budget ya miezi 2 mbele na mkewe hana, kanifuata kuniomba ushauri.Mi ni kamwambia si urudi kwenye boda boda pikipiki si unayo kumbe hela alienda kujengea.Hii ni tofauti ya kuzika hela na kutumia pesa kutengeneza pesa
Sasa huyo alikuwa 26 yrs sijui wewe una umri gani ila plan za kuingiza hela ni muhimu sana kuliko kuzika hela wkt huna sehemu za kuingiza pesa za uhakika