Nashauri tumsamehe bure Mzee Msekwa kwa kuwa siyo kosa lake. Chadema ndiyo chama cha kulaumiwa kwa kuwa kinawapeleka mbio wazee waliozeeka kiasi cha kushindwa kufikiri vizuri. Uwezo wa kufikiri ndani ya CCM umepotea na sasa wanafanya mikumbo tu. Watu waliopora mabilioni ya nchi utawaadhibu kwa kuwafukuza Kamati Kuu halafu utarajie kuonekana umetakasika mbele ya wananchi walioamka kweli? Waandamanaji wangapi kule kanda ya ziwa wanajua Rostam alikuwa mjumbe wa kamati kuu? Wangapi wataona tofauti kati ya Chenge aliyekuwa katika kamati na huyu aliyetoka? JK, Msekwa wote vituko tupu.
Kwenye
red, unajua tatizo walikuwa nalo ni uchu wa madaraka wakasahau watu wanabadilika kimitazamo na kifikra pia kuna kizazi kisichojua
ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI. Wenzao wenye akili walipoona umri unawatupa wakaachia ngazi.
Si unakumbuka alama zilionyesha kuwa hatakiwi kwenye uspika wa Bunge la 2005-2010, kwa kiburi akatia jina lake pamoja na kushauriwa asifanye hivyo. Sasa ile chali kama ya mende aliyopewa na Sitta utasema walileta CHADEMA?
Alipokuwa madarakani alisahau kuna uzee, hakujiandaa. Matokeo yake akawachukia wana-ukerewe, mbunge wao mpaka mazingira ya visiwa vile.
Kwenye
blue, wapo wana-CCM wengi waliovichwa, tatizo makundi yamewaweka kando. Na hata wakitoa ushauri wanaambiwa wehu, wanakisirani ama wanawivu. Matokeo mwenye akili hawezi kuwa pamoja na hawa walafi akajipunguzia heshima yake.
Fikiria, kumfanya Tambwe Hiza kuwa mtu wa propaganda, Je! Inamaana CCM wameishiwa tanks zao zote zilizozalishwa Kivukoni?
Tumjadili akiwa hai huyu mzee. Tukimjadili wakati anaitwa marehemu watatuambia si wastaarabu, nk kwasababu tunamchambua alivyokuwa hai.
TWENDE KAZI!!!