Kwa uelewa wangu mdogo, Kuna sababu kadhaa nzuri na mbaya, zenye maslahi kwa taifa na ambazo hazina maslahi, za kugawa mikoa na wilaya. Ukweli ni kwamba sababu iliyo nzuri ni ile ya kuboresha au kurahisisha ufikishaji wa huduma kwa wananchi. Pia, si unajua kuwa JK anapenda kulipa fadhila kwa awapendao hata kama ni mafisadi; hiyo amegawa mikoa na wilaya ili hatimaye apate kazi ya kuwapa rafiki zake pindi akishinda uchaguzi (ingawaje mwaka huu kidogo hali kwake na wabunge wake si rahisi kama ilivyokuwa 2005). la mwisho, hii nimbinu ya kusababisha hata kuongeza majimbo ya uchaguzi ili kujaribu kuhakikisha kuwa nguvu ya CCM haipungui hata wakati viti vingi vitakuwa vimechukuliwa na chadema.
Kidumu chama ya Demokrasia na Maendeleo!