(1)UVIVU
Kiini kikubwa cha umaskini wetu ni UVIVU. Watanzania wa leo hasa vijana hawapendi kufanya kazi ngumu. Wanapenda sana starehe na maisha ya luxury bila kujua kuwa maisha hayo huja baada ya kuhangaika kwanza.
(2)ELIMU/MAARIFA.
Watanzania tuliowengi hatuna ujuzi/maarifa ya UBUNIFU.
Pamoja na serikali kutumia fedha nyingi sana kugharimia ELIMU, lakini hatujapata maarifa ya kuweza kujiendesha wenyewe.
Mimi nilitarajia kuwa, ndugu zetu wasomi wanaohitimu vyuo vikuu kila mwaka wangeweza kuwa msaada mkubwa katika jamii hasa katika kipengele cha UBUNIFU.
Kinyume chake, mtu anahitimu chuo kikuu lakini bado anakuwa tegemezi kama mtu mwingine yeyote yule ambaye pengine hana hata elimu ya kutosha.
Ndipo utakuta unapotafuta kazi wewe mwenye elimu ya kiwango kidogo mnakutana na mtu wa chuo kikuu naye anatafuta kazi badala ya yeye kuwa MWAJIRI.
MAPENDEKEZO KWA SERIKALI.
(1)Kabla ya kupewa mkopo wa kusomea Chuo kikuu, kila mwombaji afanye yafuatayo:-
(i)Aeleze ni nini anakwenda kusoma na anatarajia kupata maarifa gani?
(ii)Maarifa atakayopata atayatumiaje ili kuleta ufanisi kwa ajili yake yeye mwenyewe, jamii na Taifa kwa ujumla?
NB:-Mkopo apewe atakayekuwa ametoa mchanganuo wenye mtiririko na mantiki inayoeleweka vizuri.
(2)Serikali ifungue mashamba makubwa na kujenga MAKAMBI ya kutosha na ipeleke zana na pembejeo za kilimo.
Baada ya hapo serikali itafute WAZURURAJI wote nchi nzima na kupelekwa kwenye MAKAMBI hayo kwa lengo la kuwafundisha kazi. Wakae kwenye MAKAMBI hayo kwa muda wa miezi 6, kisha waruhusiwe kurudi kwao wakibadilishana zamu na WAZURURAJI wapya.
(3)Serikali iongeze UKALI hasa kwa watu wanaoendekeza uzembe kazini.
Hata kutumia UDICTATOR kiasi kwa lengo zuri la kuleta maendeleo katika nchi siyo dhambi.