Nini Mstakabali wa Taifa Letu

Ikimura

Member
Apr 1, 2011
22
2
Kwa kipindi kirefu sasa nimekua nikitafakari ni wapi sisi watanzania tunapoelekea, nimekua sipati jibu la moja kwa moja. Toka Mh. Jakaya aingie madarakani yametokea mengi na hayo mengi ni yakutisha na kusikitisha vilevile. Ni kirejea manene ya baba wa taifa kuwa kila zama na mambo yake,na kinachotakiwa kufanywa na wananchi ni kuchukua mazuri na kuacha mabaya. Ila ukiangalia kwa undani zaidi zama hizi za Mh. Kikwete zina mabaya zaidi ya mazuri kama yapo sasa hapa angekuepo baba wa taifa labda tungeweza kumhoji tuchukue lipi hasa zuri kwa Mh. kikwete.

Nitafanya uchambuzi hasa kwa mambo yanayotokea sasa katika taifa letu hili. Tanzania limekua taifa la kila mtu kujiamlia afanye nini bila ya kuogopa chochote.Nenda kwenye ofisi nyingi za serikali utakuta mfanyakazi wa chini anaongea kama boss na haogopi na haijalishi kama yeye ni msemaji au si msemaji. Hapa si maanishi kuwaziba mdomo wale wanao tetea maslai ya wengi la hasha bali ninaongelea wale wafanyakazi wanaopata "promotion" kwa kubebwa, utamkuta ofisini hana kazi ukimwambia akupishie barua atakwambia ana kazi, na ukibishana nae kidogo anakwambia sipitishi nenda kokote uendako. Cha kustajabisha huyo mfanyakazi si wa cheo cha kukwambia nenda popote pale, ila kwa sababu amewekwa kwasababu ya maslai ya mkubwa fulani basi atajifanya yeye ndio mkubwa.

Lakini vilevile utendaji wa wizara zetu na mawaziri wengi si mzuri. Waafrika na hasa watanzania ni wanafiki, na tumekua hatujiwezi mbele ya shilingi, ukimwonyesha mwafrika shilingi basi ulimi utamtoka mithili ya mbwa mwenye njaa aonapo nyama. Hili naliongelea kwa mawaziri Sitta, Mwakyembe na Magufuli. Mawaziri tajwa hapo juu wamekua wakionekana na wengi kama watetezi wakubwa wa wananchi na mimi vilevile nawaona hivyo ila nitafurahi zaidi watakapo jiuzulu nafsi zao kwakuwa tu Serikali imeziba pamba masikioni na haitaki kuungana nao kuwatetea wananchi, kama hawawezi kujiuzulu mimi nitawaona kama wanafiki kwa sababu wanapigania haki ndani ya uthalimu, na kwa hiyo sasa wanaonekana kama watu wasiotaka kuachia posho na marupurupu ya uwaziri. Katika utendaji kunakitu kinaitwa "collective responsibilities" na kama baraza la mawaziri limejadili chini ya mwenyekiti wake na likafikia maazimio then, kama waziri haridhiki na maazimio yale then the best thing for that minister ni kujiuzulu. Mh. Sitta ametoa kauli nzuri sana kwa mfululuzo ndani ya miezi ya hivi karibuni na iliyo nifurhisha zaidi ni ile ya wananchi kukata kuburuzwa na kikundi cha watu wachache ambao hawazidi hata kumi na kuwapa miaka miwili la sivyo tuwakatae. Hapa naungana na Sitta, ila ninamtaka atoke huko ndani ili aje aungane na sisi ili tuweze kuwaondoa hao mafisadi wasiozidi kumi madarakani,ila kwakuendelea kwake kukaa nao (hao watu wasio zidi kumi) then, nae anaonekana mmoja wao. Magufuli nae amekua akikinzana na Raisi na Waziri Mkuu, hawa wawili maekua wakimwaibisha hadharani, sasa mimi kitu ambacho si kielewe ni kuwa nini hasa ambacho bado kinamshikilia magufuli kwenye uwaziri ni posho na marupurupu au? Kwa sababu baadhi ya mambo aliyoyapanga kuyatekeleza kama waziri yamesitishwa.

Kuhusu mafisadi, hili linanisikitisha kwa sababu watu ambao wanatuibia baadhi yao hata sio weusi kama sisi. Hapa mimi sitaki kuleta dhana ya Ubaguzi wa rangi ila mtu kama yeye ni Mtanzania mwenye asili ya Kiarabu au Kihindi na hataki kujiona kama yuko sawa na sisi watanzania wenye asili ya kiafrika then nafikiri huyo mtu afukizwe aende kwa watu wanae fanana nae wahindi na waarabu ni watanzania wenzetu ila wamekuwa wakitudharau na kutuibia kwa muda mrefu ifike wakati sasa tuseme basi hata kama umezaliwa kijiji kipi kama wewe huwezi kuishi kama sisi bora urudi kwenye asili yenu. Na waafrika wenzetu wanaoshirikiana na wazungu, waarabu na wahindi kutuibia, mwisho wao utafiki pale watanzania watakapo sema basi mtabaki mnahaha kama majogoo, muulize Ben Ali alipo enda ufaransa kusaka hifadhi walimkataa japo alikua akila nao.

Jamami Tanzania, Wanajamii, Maskini wenzangu, wakati ni huu
 
Mustakabali haueleweki, ona jinsi vyombo vya habari vilivyotekwa na suala dogo la tiba ambayo hataijathibitishwa, vita dhiti ya ufisadi vimehamia loliondo. Serikali yenye ipo likizo kwa sasa na mafisadi wanapumua, hakuna cha Dowans wala Richmond tena. Sasa ni Loliondo kwa kwenda mbele.
 
Mkuu, hivi sasa nchi yetu imezingirwa na giza nene hakuna yeyote ajuwaye ni wapi tunakoelekea. Kwa maoni yangu nchi yetu imetumbukia kwenye giza hili taroro hasa kutokana na katiba mbovu inayompa madaraka makubwa sana kiongozi wa nchi na serikali, kiasi cha kumfanya kuwa sawa na mungu mtu. Hivyo hatua ya kwanza inayotakiwa kuchukuliwa ili nchi yetu iweze kujikwamua katika janga ili, ni kuanzisha mfumo wa utawala ambao unazingatia msingi wa "checks and balance." Kutokana na sababu hiyo wale wote wanaolipigia danadana suala la katiba mpya hawaitakii mema nchi yetu.
 
Msatakabali wa Taifa letu anao kila mtanzania ukiwemo ww. Timiza wajibu wako kwa juhudi na maarifa.
 
Back
Top Bottom