Nini mchango wa final year projects za wanafunzi elimu ya juu kwa taifa?

Moneyowner

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,423
1,251
Ndugu zangu ukisema elimu ya chuo kikuu , unapata picha ya elimu ya hali ya juu sana,ambayo pamoja nakwamba inampa hadhi mtu binafsi lakini pia ni manufaaa kwa taifa. kwa sasa ninavoiangalia elimu yetu sana inazidi kudidimia kwa kuwa ilishazama tangu zamani.


ndugu zangu unaposema 'FINAL YEAR PROJECT' inalenga kuleta ufumbuzi na ugunduzi wa mambo mbalimbali,ni dhahiri kabisa nchi hii ina matizo mengi ambayo yanatakiwa yatafutiwe ufumbuzi na hawa wasomi. mara nyingi watu wamekuwa wakifanya project ambazo zilikwisha kufanywa. na project nyingi ni more theoretical ni mtindo wa COPY AND PASTEProject nyingi hazina implementation , theory ndio nyingi. swali kwa MAPROF mnafundisha nini ndugu katika fani mbalimbali na zaidi katika uhandisi ,science na uchumi. nilitegemea kuona matunda mazuri kutoka kwa hawa vijana wanaomaliza'

inasikitisha kijana anamaliza chuo ikuu hana jipya mbali na kwenda internet kukusanya data kuziweka pamoja then kusbmit as a final year project , naye prof kuipokea na kuiweka kabatini na kusahau kabisa. kwa hiyo shule inakuwa kama njia kuelekea kupata ajira basi. hakuna asiyependa kazi yenye hela nzuri ,lakini watu wanamaliza fisrt degree, masters na PHD. siyo rahisi kusikia jambo kubwa kutoka project zao za mwisho wa masomo.

SWALI: KUNA HAJA YA KUFUMULIWA MFUMO WA ELIMU TZ?
 
Back
Top Bottom