Nini madhumuni ya uwepo wa binadamu?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Ninafahamu akili aliyonayo binadamu inamfanya kupambana na mazingira yanayomzunguka na kutokana na mapambano hayo, ndiyo maana uvumbuzi wa vitu mbali mbali umetokea.

Binadamu tunapojikuta tupo katika mazingira fulani ni kawaida kutumia akili ili kupambana na mazingira hayo.

Binadamu hatukupewa uwezo wa kuchagua kuwepo au kutokuwepo katika mazingira ambayo tunajikuta tumewekwa na Mungu au mabadiliko ya kimaumbile (evolution).

Ninaamini kama tungekuwa tunapewa uwezo wa kuamua, kuna wengine wangeamua kutowepo katika dunia na mbaya zaidi, kujiua au kuua binadamu imekatazwa na aliyetuweka (Mungu) na pia tumekatazwa kwenye sheria zilizowekwa na waliotutangulia kwenye mabadiliko ya kimaumbile (evolution).

Kwa wale watalaam wa vitabu vya Mungu, kwa nini Mungu aliumba binadamu? Kwa nini alituumba na kutupatia sheria ambazo zinazifunga fikra zetu katika maamuzi?

Kwa wale Wataalam wa dhana ya mabadiliko ya kimaumbile (evolution.), nini dhumuni/madhumuni ya uwepo wa mabadiliko ya kimaumbile yaliyosababisha uwepo wa binadamu? Kwa nini hatuwezi kuona mabadiliko ambayo tunaweza kuamua kuwa katika maumbile tunayopenda?
 
Mwanadamu ameumbwa na Mungu ili Kumwabudu na kutii amri zake.
Huoni kama kuna binadamu wengine wamelazimishwa kufanya jambo ambalo kama wangeulizwa kama sharti kabla ya kuumbwa wangekataa kuumbwa binadamu.

Huoni kama hawakutendewa haki na Muumba?
 
Huoni kama kuna binadamu wengine wamelazimishwa kufanya jambo ambalo kama wangeulizwa kama sharti kabla ya kuumbwa wangekataa kuumbwa binadamu.

Huoni kama hawakutendewa haki na Muumba?
Hapo pia kwa upande mwingine inabidi ujiulize kwa nini umekuja duniani bila mapenzi yako? Je ni nani amekuleta? Kama jibu litakuwa Mungu ndio kakuleta basi lazima umtumikie yeye na kutii amri zake. Kama unaamini evulution, basi jiulize kwa nini hiyo evulution imesimama isiendelee? Sababu viumbe vilibadilika mpaka akatokea binadamu wanavyo sema, lakini binadamu hajaendelea kubadilika na kuwa kiumbe kingine japo anapambana na hali ngumu.
 
Huoni kama kuna binadamu wengine wamelazimishwa kufanya jambo ambalo kama wangeulizwa kama sharti kabla ya kuumbwa wangekataa kuumbwa binadamu.

Huoni kama hawakutendewa haki na Muumba?
Kwanza kabisa dhana ya maamuzi iko katika hali ya utambuzi, utambuzi upo katika uwepo( essence), hivyo uwepo wa mwanadam ni sheria asilia (law of nature) ambayo ni sawa na kusema ni Mungu (supreme being) hivyo mwanadam hana uchaguzi wowote juu ya uwepo wake, pia asili imeweka ukomo wa uhuru wa mwanadam ambao humuweka katika maono ya utumwa, hata hivyo mwanadam akikiuka ukomo huu hujikuta katika matatizo.

Mungu alimuumba mwanadam ili kutimiza (siku sita ya saba akapumzika) utukufu wake, mwanadam yapaswa kumwabudu Mungu
 
Kumbe amri za Mungu za kumtii yeye tu zinaweza kupingwa na mwanadamu, mbona sasa waovu ni wengi kuliko wema, ina maana Shetani ana nguvu kuliko Mungu?
La hasha si kwamba ibilisi ana nguvu kuliko Mungu, kumbuka mwanadam ana asili ya matamanio, matamanio hayo yaliyo mengi yameegemea katika uovu ambao Mungu haupendi, shetani hutumia mwanya wa tamaa za mwanadam ili kumshawishi aende kinyume na Mungu, pia Mungu ameonyesha upendo kwa binadam ili watende wapendavyo ili kila matendo ayalipe kwa kadri yake, kama ni uovu atamlipa aliyeutenda, pia kama ni wema atamlipa kwa kipimo chake.
Ufuasi kwa shetani ni matokeo ya dhambi kuendana na tamaa za mwanadam kama vile, ulafi, ufiraji, wivi, uasherati, uzinzi, ufisadi, uongo, uuaji, n.k hayo yote yanarahisisha shetani kuvuna wanadamu wengi.
 
Kumbe amri za Mungu za kumtii yeye tu zinaweza kupingwa na mwanadamu,
Mimi sina tatizo kuhusu binadamu ameumbwa na nani, tatizo langu ni ridhaa kwa yule aliyeumbwa kutoka kwa muumbaji na dhumuni lake ni nini kumuumba bila ridhaa yake.
mbona sasa waovu ni wengi kuliko wema, ina maana Shetani ana nguvu kuliko Mungu?
Hapa hatuwezi kufahamu kama watenda maovu ni wengi kuliko wema labda kama kuna utafiti ambao umefanyika.
 
Hapo pia kwa upande mwingine inabidi ujiulize kwa nini umekuja duniani bila mapenzi yako?
Nimejikuta nipo duniani na katika nazingira hayo nimejikuta najiuliza, dhumuni la kuletwa hapa duniani bila kuulizwa nini?
Je ni nani amekuleta? Kama jibu litakuwa Mungu ndio kakuleta basi lazima umtumikie yeye na kutii amri zake.
kwa nini nitakiwa nimtumikie yeye wakati hakunipa nafasi ya kuchagua kabla hajanileta duniani.
Kama unaamini evulution, basi jiulize kwa nini hiyo evulution imesimama isiendelee? Sababu viumbe vilibadilika mpaka akatokea binadamu wanavyo sema, lakini binadamu hajaendelea kubadilika na kuwa kiumbe kingine japo anapambana na hali ngumu.
Kusimama au kuendelea kwa evolution siyo msingi wa hoja yangu, ninachotaka kufahamu kwa nini evolution haikutoa/haitoi nafasi ya kuchagua kabla ya kama ninapenda kuwa katika umbo la binadamu au la
 
Nimejikuta nipo duniani na katika nazingira hayo nimejikuta najiuliza, dhumuni la kuletwa hapa duniani bila kuulizwa nini?
kwa nini nitakiwa nimtumikie yeye wakati hakunipa nafasi ya kuchagua kabla hajanileta duniani.

Kusimama au kuendelea kwa evolution siyo msingi wa hoja yangu, ninachotaka kufahamu kwa nini evolution haikutoa/haitoi nafasi ya kuchagua kabla ya kama ninapenda kuwa katika umbo la binadamu au la
Ndugu MsemajiUkweli kupata majibu ya maswali yako ni ngumu sana, sababu ya kwanza ni kuwa huna kumbukumbu yoyote kama ulikuwa sehemu ukajikuta upo dunia katika umbo la kibinadamu bali umepata akili ukajikuta upo hivyo. Pia hayo mambo yote unayo hoji huku ya jua, bali ni baada ya kusimuliwa na hapo ndio ukajenga hayo maswali. Jaribu kufikiria kama ungezaliwa na kuwekwa duniani peke yako pengine usinge kuwa tofauti na wanyama, ungekisia tu hiki kitu kinaweza kunidhuru na kikinidhuru kita tokea nini sana sana maumivu. Ungejua kuwa pia kuna kifo? hatujui, au ukifa hurudi tena? hatujui. Sababu tunao ogapa kifo ni sisi tunao ishi, walio kufa hawajui hilo tena. Na kwa nini tunaogopa? Sababu tunajua ukifa hurudi tena. Nini kinaendelea ukifa, hapa ndio sasa tunapata habari za uwepo wa Mungu. Je tuamini kuwa Mungu yupo? hapo ndipo shida inakuja. Lakini kwa upande wako unaamini yupo, ndio maana unauliza kwa nini hukupata nafasi ya kuchagua uwe katika umbo gani? Nani huyo angekupa nafasi ya kuchagua? Kama yeye alikuchagulia basi anakusudi na wewe? Sawa na rais anapoteua mawaziri sababu hawapi muda wa kuchagua wizara, lakini kwa kuwa wanaamini wameteuliwa na mamlaka iliyo juu yao mara moja wanaukubali uteuzi huo na kuanza kuutumikia.
 
kabla ya kuuliza madhumuni ya uwepo wa binadamu,tujiulize kwanza nini
madhumuni na uwepo wa maji,miti na pepo zinazunguka dunia hii pande zote.
 
Kuhoji madhumuni ya mwanadamu inabidi kwanza kuhoji uumbaji kwa ujumla na kila kitu kilichomo
Siwezi kuvisaidia viumbe vingine kuhoji kwa sababu sifahamu makubaliano yake na Muumba wao.

Nitakuwa sivitendei haki au nikakuwa mnafiki kwa sababu hoja yangu ina msingi wa uhuru wa kuchagua.
 
Mimi sina tatizo kuhusu binadamu ameumbwa na nani, tatizo langu ni ridhaa kwa yule aliyeumbwa kutoka kwa muumbaji na dhumuni lake ni nini kumuumba bila ridhaa yake.

Hapa hatuwezi kufahamu kama watenda maovu ni wengi kuliko wema labda kama kuna utafiti ambao umefanyika.
Labda ungetwambia wewe kwa nini uko duniani!

Kwa kuwa umo duniani unafanya nini!

Usipokuwepo duniani kitatokea nini.

Ujibu tofauti na vitabu vya dini (biblia/quran) ambavyo kimsingi ni imani.
 
naam!! kuna wakati huwa najiuliza kama nadharia ya uumbaji ni kweli kwanini mungu aliamua kuumba ulimwengu?. uwepo wa binadamu unafaida gani kwa mungu? kwanini mungu asimmalize shetani anaye tuhumiwa kushawishi uovu miongoni mwa binadamu? kwanini hawasiliani na watu moja kwa moja? kwanini wanadamu wote walipie makosa ya adam na eve?
 
Mbona majibu nayaona ya upande mmoja tu kwa waumini wa dini,ina maana hao wengine hawana majibu kwa hili swali?
 
Back
Top Bottom