Kila charger ina specs zake, na ni maalum kwa kifaa husika. Kwanza cha muhimu ni output voltage na current. Kama simu/kifaa chako kinahitaji input ya 5V, 800mA. Then wewe ukatumia charger yenye output ya 7V basi unahatari ya kuunguza kifaa chako,.
Ingawa kila simu ina inbuilt voltage regulator, lakini pia hizo regulator zina specific input range.
Cha pili, charger zisizo original zimeandikwa specs za uongo. Unakuta chaja imeandikwa output 5v. Lakini ukiipima unakuta 10v
Voltage ni lazima iwe sawa sawa, lakini current (Ampere) inatakiwa iwe sawa au izidi kidogo. Kwasababu voltage inasukumwa na chaja kuingia kwenye simu, lakini current haisukumwi bali simu inajichukulia kiasi chake yenyewe kinachotosha.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.