Nini madhara/ faida ya bangi?


Mkuu OMEGA uko sahii kabisa mi kuna vijana nilisoma na wengine nimekua nao mtaani wao waliona bangi ndio ujanja...sasa shule iliwashinda maisha wamepigika matokeo yake siku ni kunitia mizinga ya buku buku kila siku yahani sina hata amani asubuhi nikiwa naenda job au jioni nikirudi...washikaji tunaringana umri ila wanaanza kukuita bro...ganzi sio kabisa ila ni bora mara mia ya poda
 
Last edited by a moderator:

Bangi ni kweli sio nzuri, ila utafiti wako umekosea kwa kusema asilimia kubwa ya watumiaji unaowafahamu wamewehuka sababu ya bangi. Hiyo tafiti ina walakini. Mf. Tatifi za pombe kwamba zinamaliza maisha ya watu kwa vifo..ni kweli ila hakuna tafiti ya kuonesha ni watoto wangapi wanazaliwa kwa sababu ya pombe hiyo hiyo! Rate ya vizazi na vifo vinavyosababishwa na pombe ni ipi kubwa?

Kila kitu ni kwa kiasi, ndioml maana wanaohalalisha bangi wameweka kwa ajili ya tiba na utabibu so wanatumia kiafya na kwa uangalizi maalum.


Bangi haihitaji stress..so mvutaji anatakiwa awe ametulia kiakili,pia awe well financially mambo ya vyakula na maji hasa matunda kwa wingi.sasa ukijumlisha stress na kutobika mifuko mtu lazima achizike.

Hao unao ona wamedata mtaani ni asilimia ndogo sana ya wavutaji.wengine utashangaa ukiwaona au ukijua kuwa ni wavutaji.

Bottom line bangi ni nzuri, ila si nzuri kwa wote.
 

Tehe teheh umenifurahisha sana. Hivi ukiruhusiwa huo mjani si patachimbika au ni fikra zangu tu?
 
Mmhh, mtu anakula 'the herb of all times' afu anashindia skonzi na soda na hana kazi yuko kijiwezi anapiga stori tu, lazima adate.
Bangi bila menyu na kufanya kazi ni kujitafutia kichaa cha bure.

Uko sahihi kabisa mkuu.
 
Huwezi vuta bangi afu ukashindia soda ukabaki sawa

Donts za bangi, ka,a mvutaji.

1. Lazima ule chakula cha kushiba na chenye nguvu
2. Lazima ufanye kazi, kuunguza bangi uloivuta
3. Lazima uweke wazi kwa wanaokuzunguka kuwa wewe ni mvutaji. Kimtu kinavuta bangi afu hata kwao hawajui kama kinavuta afu kinategemea kibaki sane? Majanga
4. Lazima uwe na ratiba, sio unavuta tuu kama unakunywa chai
5. Ujue historia ya ukoo wenu, kama unaendana na bangi. Koo zingine vichwa panzi, hata wakienda tu high skul wanadata.
6. Lazima ujue stail bora ya usokotaji, na uvutaji. Kuvuta kwa kiko cha maji ni nzuri zaidi.

 

nimependa uzoefu wako, nitakuja unifundishe jinsi ya kunyonga mjani kwa afya:A S thumbs_up:
 

Bob Marley alikuwa ni mvutaji mkubwa wa bangi but alikufa kwa kansa!! Mh!! Hapo kwenye bold hapo!!

Niliacha kuvuta bangi baada ya siku moja jamaa yangu kuvuta na akachaanganyikiwa akawa kama kichaa kabisaaa within a minutes. Tulimpeleka kwao tukamkuta dada yake home tukamwambia jamaa anaumwa na kichwa apumzike, dada alikuwa anakata kabichi ili apike mboga!! Jamaa alikula kabichi mbichi yooote mpaka ile ambayo ilikuwa haijakatwa kama nguruwe hadi dada mtu akaogopa sana akatutafuta tukamzingua ni homa tu hizo na vitu kama hivyo.

Tangu siku hiyo niliapa kutokuipitisha tena bangi usoni mwangu, namshukuru Mungu nilifanikiwa sana
 

Na uwakumbushe watoto wa ki sure wanaokula bangi ila hawajui kunyonga bora waache manake wahuni wana mix na mambo yao so wakivuta dope wanachizika wanadai ni bangi kumbe crack.

Eat what u kill urself! Ndio sharia ya ganja.
 
Navuta bangi mwaka wa saba huu....bangi ni poa sana......inanipa raha ya kipekee sana....inanipa utulivu wa akili na mawazo......inanipa hamu ya kupiga kazi kwa bidii kwa maana hiyo nimetimiza malengo yangu mengi sana kupitia bangi..... I LOVE YOU BANGI AND I WILL NEVER LEAVE YOU.......
 
unajua hebu jaribu kujiuliza maswali ya ufahamu,ni nani aligundua bangi na nani akagundua matumizi yake??????ukipata majibu sasa endelea na utafiti wako,but kwa upeo wangu mimi all human are created with the nature of GOD i mean uungu,sasa god's nature can not exit without third eye,hivyo kaa ukijua watu tabaka la juu hawawezi kuruhusu uhalali wa bangi kwasababu wanajua faida iliyopo kwenye bangi.
 
mfano mzuri mimi nimesoma GALANOS ckufichi yani kuna jamaa yangu alikua anapiga bangi mpaka akapewa jina kayaman from kingstone jamaika,sasa cha ajabu yule jamaa alikua na nguvu za ajabu sana yani namaanisha uwezo tofauti,alikua PCM na ukimfuata kabla hajavuta hawezi kusolve na alipiga kijiti tena cha single digit akapangiwa ifunda tech form5.
 
kwa ufupi ni kwamba kuna kitu kinaitwa third eye awakening,sasa hii kitu inahusiku hapa na ukitaka kuprove chunguza kuna wavuta bangi wakilala usiku wanawaona wachawi lakini asipovuta bangi haoni,hii ni kwasababu bangi ni mmea asili unaoamsha nguvu asili yani jicho la tatu(uungu) na ndio maana freemasons hawatak kuiruhusu huku wao wakiendelea kuitumia.
 
ufafanuzi zaid freemasons is not connected to GOD's nature that is atificial power(man made thing) usije ukachanganya mabo hapo
 
Hello,

Nime-observe wengi wanaovuta bangi wanakuwa wakorofi sana, na wababe hivi kuna uhusiano wowote kati ya kuvuta bangi na kuwa MTU wa mabifu??

Kwa wanaovuta bangi au wanaojua kuhusu hili wanijuze...
 
Hello,

Nime-observe wengi wanaovuta bangi wanakuwa wakorofi sana, na wababe hivi kuna uhusiano wowote kati ya kuvuta bangi na kuwa MTU wa mabifu??

Kwa wanaovuta bangi au wanaojua kuhusu hili wanijuze...
Kwani kuna wavuta bangi humu?.
 
Uhusiano upo kabisa, wanasema huwa inakupa Nguvu bandia na uwezo wa kujiamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…