Nini maana ya PF 3.

Nini maana ya PF 3.

famba

Member
Joined
Mar 21, 2013
Posts
71
Reaction score
4
Nilikuwa na mgonjwa aliyepata ajali ya pikipiki, kila hospitali ninayoenda hawataki kumtibu wanasema mpaka PF 3 na hii case ni ya Amana, jamani mpaka mgonjwa afe!!! Nini maana ya hii PF 3????
 
PF 3 ni polisi form namba 3 ambayo dakitari hujaza maelezobya mgonjwa kwa ajili ya michakato ya kesi hapo baadae.
Hao madaktari wa Amana wamefanya kosa sana maana kwa utaratibu mpya walitakiwa wampe tiba wakati PF 3 inafuatiliwa hauwezi kumuacha mgonjwa afe kwanza ni kinyume cha kiapo cha udakitari.
 
Hao Madaktari watamtibu tu wakati PF. 3 ikifuatiliwa, unachotakiwa waeleweshe vizuri
Mfano ajalizote za mabasi au magari na pikipiki sijawaiona wakiitaka PF. 3 kwa abiria 65 ndipo wawatibu, na kwa ajali ya pikipiki lazima mpo zaidi ya mashuhuda wa2
Tatizo linakuja km Mgonjwa kadungwa risasi (kitu chennye ncha kali) huenda alikuwa jambazi, huenda anatafutwa kwa kuvunja mahali nk hii husaidia kuwadhibiti wahalifu wasitibiwe
 
Umejibu vyema ila sio daktari tu anayejaza isipokuwa hiyo fomu hujazwa kwanza na polisi akieleza kilichotokea kwa mgonjwa/majeruhi maana ikienda plain daktari hawezi kukuelewa,
 
PF 3 ni polisi form namba 3 ambayo dakitari hujaza maelezobya mgonjwa kwa ajili ya michakato ya kesi hapo baadae.

Huko huko polisi pia hutolewa kitu kinaitwa RB hasa pale mtu anaporipoti kupigwa ama kudhulumiwa na mtu fulani. Je maana ya RB ni nini??
 
Back
Top Bottom