Nini maana ya ndoto hii?

Nini maana ya ndoto hii?

Joined
May 24, 2015
Posts
19
Reaction score
10
NDOTO YANGU....
Ilikuwa ni saa 20:17 nilipanda kitandani mpaka kufikia dakika ya 12 toka nilipo panda kitandani ...nilikuwa tayari nimekwisha shikwa usingizi...ghafla ndoto ya ajabu ilikuja ndoto hiyo nilishindwa kuitafasili .

Nikiwa ndotoni nilipata kuona ufalme mzuri uliopendwa na watu Sana'a utawala huo niliufananisha na mtoto mdogo ampendae mama yake , ufalme huo ulipata jina na ulikuwa ukijiita ufalme wa kondoo na muda wote ulijinasibu kwa kutenda mema kwa wananchi wake ......baaada ya miongo miwili ufalme ule ulianza kufanya mambo kinyume na matakwa ya watu wake wengi ...

Ufalme mkongwe uliokuwa jilani huu ulijulikana kama ufalme wa moto ufalme huu ulikuwa ukifanya yale vitabu na maagano vilielekeza vifanye ...kwa sababu utawala wa moto ulikuwa na majukumu ya kukosoa ufalme wowote
Japo kuwa ufalme wa moto ulionekana hauna nguvu za kijeshi lakini misingi iliyokuwa imejenga kwa watu wake ilikuwa misingi ya kupendwa na kuaminiwa na watu wake sanaaa yaani tunaweza ita ufalme huu kuwa ni ufalme wa imani..

Ufalme wa kondooo ulifika wakati ukabadilika na kuwa ufalme mkolofi na wanachi waliokuwa wanaupenda wakawa wanauliwa ovyo, oyo, wengine wanateswaa na waliobaki salama ilibidi wajifanye wanautukuza na kuupenda huku wakiwa na hofu ya kuteswa kama wenzao...

Kimsingi ulipata vibaraka wengi na wengi walishidwa kutoufata ufalme huo kwa hofu ya kupoteza maisha, kupoteza Mali na hata kukosa msaada wakati wa matatizo...hivyo ufalme huo ukabadilika na kuitwa ufalme wa dubu......ufalme huo ulitikisa mataifa jilani na hata mataifa matatu makubwa yaani falme tatu kubwa zilitikiswa falme hizo ni ufalme wa mawe , chuma , na hata ufalme wa maji ......

Ufalme wa moto ukachukizwa na vitendo hivyo kisha ukatuma mjumbe ukatoa maelekezo kuwa "nenda kamwambie mfalme wa ufalme mpya mkolofi na dhalimu wa dubu kuwa unayo yafanya si Yale ambayo yanatakiwa yafanywe na wafalme kwenye falme zao...ukasena wambie watu wanahitaji , Uhuru, kupendwa na kuwa salama ...lah sivyo ufalme wa moto japo hauna slaaaa utatumia nguvu ya watu iliyonao kuutawala ufalme wa dubu " ujumbe ulifika lakini wazeee wa baraza wakaandika majibu wakiueleza ufalme wa moto kuwa ..."hauwezi kuona mdomoni wangu nine shikilia mbavu tatu nikiashilia kuanguka kwa falme tatu kubwa ambazo kimsingi zinakuzidi nguvu ..naukiendelea kuufuatilia ufalme huu mpya wa dubu tutakuja kukufutilia mbali na watu wako wataishi kwenye mateso.....

Ujumbe ulifika na ufalme wa moto ulichukizwa na majibu hayo ...kwa sababu ulikuwa hauna silaha ulitumia Sera moja ya watu kuzaliana sanaaa mpaka kupelekea idadi ya watu kwenye ufalme wa moto kuwa mara mia tano ya watu wa ufalme wa dubu ...

Ndipo ufalme wa moto ukatangaza vita zidi ya ufalme wa dubu .........ghafla nikasikia hodi dah kushituka kumbe kumekucha ....sasa hebu nisaidieni nini maana ya ndoto hiii nani ufalme upi utashinda


Na Edward Aloyce Geremiah
[HASHTAG]#mtotowamamaadelina[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom