Nini maana ya Kutakasisha pesa na lengo huwa ni nini?

Tyrone Kaijage

JF-Expert Member
Jul 19, 2021
1,611
3,342
Hili neno huwa nalisikia sikia nimejaribu kufatilia ila sipati maana halisi na mtu anayetakasisha pesa anakuwa anafaidika na nini?

Uzi
 
Hili neno huwa nalisikia sikia nimejaribu kufatilia ila sipati maana halisi na mtu anayetakasisha pesa anakuwa anafaidika na nini?

Uzi

Kutakatisha pesa ni kujipatia pesa kwa njia ambayo sheria hairuhusu na kisha pesa husika ukaziingiza katika utaratibu halali wa kibiashara au mzunguuko wa pesa hizo na biashara/mzunguko huo uonekane ni rasmi na halali ikiwa ni pamoja na kulipa kodi za serikali

Kwa Tanzania sheria hii imekua ikitumika vibaya na vyombo vya uchunguzi kama polisi,TAKUKURU na hata ofisi ya waendesha mashtaka na kisha kukomoa watu kwa kuwaweka mahabusu kipindi chote kesi itakapokua inaendelea maana kwa mujibu wa sheria ya UTAKATISHAJI hii ni kesi isiyo na dhamana

Makosa mengi ambayo mamlaka za uchunguzi wanazipeleka mahakamani hua ni ama ni kukwepa kodi, kughushi, rushwa au wizi tu wakawaida, makosa ambayo yanadhamana mahakamani

Ili kosa la utakatishaji lisimame kuna hatua zake ambazo kimsingi vyombo vyetu vya uchunguzi huwa hawazingatii na badala yake kupendelea kukimbilia kupeleka kesi mahakamani na kuishia kugalagazwa

Louganis
 
Money = fedha

Laundry = kufua/kusafisha

Money laundry = kusafisha fedha

Kinachosafishwa huwa ni kichafu.

Obtaining money from illegitimate sources and use it on legitimate issues .

Examples getting money from crimes like drug trafficking and use the money on building magorofa marefuuu.

Huwa inahusisha fedha ndefu sana na siyo vijisenti tu vya hapa na pale!
 
Actually hakunaga pesa chafu kimsingi!

Imeandikwa:

“Fedha, dhahabu , mali na vyote viijazavyo nchi ni mali ya Bwana. “

Kinachogomba ni chanzo yaani source ya upatikanaji wa hiyo fedha lakini fedha yenyewe haina uchafu wowote ndio maana inatumika kama fedha nyingine halali.

Uchafu upo kwenye source ya upatikanaji wake.

Maana mfano fedha ya kutokana na uhalifu mfano wa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ambayo imepelekea kuharibu maisha ya watu na vizazi vyao, imagine!
 
Money = fedha

Laundry = kufua/kusafisha

Money laundry = kusafisha fedha

Kinachosafishwa huwa ni kichafu.

Obtaining money from illegitimate sources and use it on legitimate issues .

Examples getting money from crimes like drug trafficking and use the money on building magorofa marefuuu.

Huwa inahusisha fedha ndefu sana na siyo vijisenti tu vya hapa na pale!
Nimeipenda hii Safi Sana umeelezea vizuri..
Mkuu utakua ticha au?
 
Hili neno huwa nalisikia sikia nimejaribu kufatilia ila sipati maana halisi na mtu anayetakasisha pesa anakuwa anafaidika na nini?

Uzi
'Kutakatisha' ni kitenzi, ni neno linalotumika mbadala ya 'kusafisha'.

Yaani chafu kuwa safi, toka haramu na kuwa halali!

Pesa yoyote ipatikanayo kwa kazi haramu, biashara haramu na matendo haramu ni pesa haramu.

Sasa pesa hiyo inapoingizwa kwenye matumizi halali, kitendo hicho ni kutakatisha.
 
Kuingiza Pesa haramu kwenye matumizi halali kama kujenga nyumba kununua Gari sio utakatishaji wa fedha.

Kutakatisha Ni Ile Pesa chafu mf. Imetoka kwenye madawa ya kulevya unaiweka kwenye mzunguko wa biashara yako halali mfano. Supermarket,casino etc. Halafu inaonekana kama Pesa zako unazojengea magorofa zinatoka kwenye hako kabiashara.

Fatillia wabunge,mawaziri,wakuu wa mikoa unakuta ana kabiashara Fulani kama shule/hotel halafu Pesa Zake Za ufisadi anaziingiza humo kuzitakatisha....hotel inapata mteja mmoja ila inaonekana Ina wateja 100 Kwa siku Kumbe Hawa 99 Ni wateja hewa Na Ni Hela kutokea ufisadini
 
Haya maelezo yameshibisha uelewa wangu hasa kwenye mstari wa mwisho "hotel inapata mteja mmoja.........".
Kwamba unaonesha unaingiza pesa nyingi ili uweze kutumia zile ulizoiba?
 
Kifupi ni kuchukua pesa ambayo sio halali Yani iliyopatikana kinyume na Sheria na kuingia kweny mzunguko yaani kuitumia
 
Basi wbongo wengi makazini ni watakatishaji fedha, mfano Traffic police au!.....hii yanatofauti gani na upigaji au rushwa?
Mkuu, wengi wa wa Tanzania wakiwemo wanasheria hawaijui sheria ya utakatishaji pesa

Wanachofanya baadhi ya askari wa usalama barabarani ni kuchukua hongo/rushwa na sio utakatishaji hata kama atatumia pesa hizo kununua pikipiki au gari ya kutembelea

Kuna hatua kadhaa lazima zitimie ili tuhuma(kosa) analokamatwa/shtakiwa nalo mtu liingie kwenye utakatishaji. Na kiuhalisia kwa Tanzania hapa ni wachache wanaweza kuingia moja kwa moja kwenye mashtaka hayo

Ndio maana sasa hivi kuna watu wengi sana wametoka magerezani walipokua wanashikiliwa kusubiria kesi zilizokua zinaitwa UTAKATISHAJI PESA(MONEY LAUNDERING )

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka chini ya Mkurugenzi wake wa sasa Bwana Sylvester Mwakitalu imeona kua watu wengi walikua wanabambikiwa shitaka la UTAKATISHAJI PESA ili tu kuwanyima haki yao ya kufuatilia kesi zao wakiwa nje kwa dhamana. Kwa maana nyingine sheria ilikua inatumika kuwaadhibu watu kabda hawajatiwa hatiani na Mahakama

Makosa yaliyopo Tanzania ni pamoja na ukwepaji kodi, matumizi mabaya ya ofisi, kughushi, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, wizi nk na katu sio utakatishaji kama ilivyokua inatafsiriwa na waendesha mashtaka enzi za DPP Biswaro Mganga
 
Haya maelezo yameshibisha uelewa wangu hasa kwenye mstari wa mwisho "hotel inapata mteja mmoja.........".
Kwamba unaonesha unaingiza pesa nyingi ili uweze kutumia zile ulizoiba?
Yeah, Unakuta mtu ana sheli ya kawaida tu lakini eti "faida" ya hiyo sheli anatumia kujenga magorofa kariakoo
 
Back
Top Bottom