Mimi ninafahamu chache tu ambazo nimekuwa naziona kwa hao wanadiplomasia aidha awe balozi au waambata wao.
Mojawapo ni kinga[immunity] ulinzi kuhusu mashtaka uwapo nje /ndani ya eneo la kazi ndio maana Dr Slaa alipotaka kushtakiwa kwa kesi ya uhaini wa kubumba baada ya kupinga mkataba wa DP World alivuliwa kwanza ubalozi.
Wanafanya manunuzi ya bidhaa katika maduka maalum ya kidiplomasia ambayo bidhaa zake hazina ushuru [duty free] hii ni kudumisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi na nchi kupitia mikataba ya kimataifa ya kidiplomasia mfano duka la wananchi kawaida bidhaa yaweza kuwa $3 kule kwenye maduka ya kidiplomasia unakuta ni $1.99
Pasi maalum ambayo inawapa nafasi kuhudumiwa haraka wawapo katika majukumu yao ya kikazi na safari [fast track]
Nyingine ni posho kadhaa kama makazi, umeme, chakula, mavazi , internet na kadhalika.