Elimu bure toka chekeachea hadi F IV ni moja ya ahadi za Mh Rais,Dr John Magufuli. Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka shule zinaandikisha wanafunzi wapya kwa ngazi mbalimbali za elimu.
Ndugu yangu amemwandikisha std 1 mtoto wake wa miaka 6,shule ya msingi Kwaang'w,Halmashauri ya Mji,Babati. Huyu mzazi na wazazi wengine wamelipishwa pesa kama sharti muhimu mwanao kuandikishwa.
1: Sh 10,000 dawati
2: Sh 2,000 maji/mwezi
3: sh 2,000 mlinzi/mwezi
Amepewa risiti ya malipo hayo. Waalimu wamewaambi wazazi kuwa haiwezekani bure kiuhalisia,labda kwenye majukwaa ya siasa.

maana ya elimu bure yaani kila kitu bwerere hakuna kulipa waliolipa ni kiherehe chao tu, hapa kazi tu.
Ninavyojua huwa kuna ada na michango ya shule. Wacha tulipe michango maana ni muhimu zaidi kwa shule zetu
ni kweli mkuu, pia nafikiri ni mapema mno kwa serikali ambayo bado inatumia bajeti ya serikali ya awamu iliyopita, kutekeleza hilo..
Hii ni serikali ya Daktari wa kemia, ni serikali yenye ubunifu wa ajabu, haitegemei bajeti ya serikali ya awamu iliyopita kwa kila kitu. Mfano pesa iliyonunua vitanda na magodoro Muhimbili, haikutoka kwenye budget, kuna pesa inaokolewa kutokana na sikukuu zisizo na tija, safari zisizo za lazima, n.k.