Samahani jamani naomba kueleweshwa nini maana halisi ya asilimia ya alcohol katika kinywaji cha bia au na vingine vyovyote vyenye kuwa na alcohol. Mimi kwa ufahamu wangu nilidhani mfano unaposema 6% alcohol inamaanisha katika kila 100ml za hicho kinywaji kuna 6ml za alcohol lakini nimesikia watu wengine wakisema hiyo inamaanisha kiwango cha kimea ambacho kimegeuzwa pombe kwa maana hiyo 94% ya kimea hakijabadilishwa. Naomba wenye utaalamu na haya masuala mnisaidie tafadhali.