Nini maana halisi ya neno " UCHOCHEZI' ?

Nini maana halisi ya neno " UCHOCHEZI' ?

Joined
May 4, 2013
Posts
27
Reaction score
22
Wanaharakati, wasomi wa sheria na wanataaluma wa lugha ya kiswahili naomba mnisaidie maana sahihi ya neno "uchochezi". Nimeamua kuomba msaada huu wa tafsiri sahihi ya neno "uchochezi" ili niwe salama ninapotoa maoni na mtazamo wangu juu ya mambo mbalimbali katika jamii yetu. Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 inasema hivi: Every person-
(a) has a freedom of opinion and expression of his/her ideas:
(b) has a right to seek, receive and, or disseminate information regardless of national boundaries. Kutokana na haki hizo tulizopewa na katiba kinachonishangaza ni kwamba leo hii katika nchi yetu ukitoa maoni yanayolenga kukosoa utawala na vyombo vyake unakamatwa na kufunguliwa kesi ya "uchochezi" sasa najiuliza, useme nini ili usionekane "mchochezi" ? Katika nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa kutofautiana kiitikadi na kimawazo si uadui ni mwanzo wa upanuzi wa demokrasia na kuleta maendeleo. Watawala wetu wanapaswa kujua kuwa mitazamo na mawazo tofauti ndiyo imeifanya dunia yetu kupiga hatua ktk uvumbuzi wa teknolojia mbalimbali.
 
Uchochezi ni hali ya kuulizia VYETI VYA BASHITE
 
Angalia ile video ya Msigwa juzi channel ten ndio utajua
 
ukiwa uchi:

1.nikisema "we mjinga unatuonyesha uchi wako vaa nguo"
2.we fala unamuonyesha nani uchi wako?

3.mijitu mengine bana unamkalia nani uchi?

4. Mh/mpendwa/rafiki umesahau kuvaa nguo

Nadhani no. 4 imekaa kiafrika, haina lugha kavu

unapozungumzia uchochezi ni maada pana, yenye culture,heshima ya kiafrica, kuheshimu wakubwa na nafasi zao

ukitafsiri hayo maneno kama yalivyo usisahau pia katika maneno yako...kuna

1.tone
2.body language
3.how,where,when and audience that receive your meseji


otherwise utalalamika, utasema jambo, utakamatwa, tutakuja segerea kukuletea uji


Pia usisahau jamii ya kiafrica ni changa mno......hao wamarekani wameishi maisha yetu mwaka 1650s...!!! ooh Yes.....hizo demokrasia ki ukweli hazipo africa, wala usijidanganye

hazipo ccm, hazipo chadema, hazipo cuf, hazipo makanisani, hazipo misikitini, wala hazipo kwa baba ako

mjue hilo
 
Uchochezi kwa tafsiri halisi ni kutumia haki yako ya kikatiba ya kuchagua upande na kuipinga ccm .
 
Uchochezi upimwa kwenye mkojo according na ndugu zetu wa kijani.
 
Subiri ukikamatwa ndio utajua maana yake,
 
Back
Top Bottom