Nini kitatokea endapo Rais atafanya hivi?

Nini kitatokea endapo Rais atafanya hivi?

kabon14

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2016
Posts
1,233
Reaction score
871
Habar za mida wakuu..

Kuna kitu najiuliza kuhusu kinga dhidi ya mashtaka anayopewa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kikatiba.

Katika nchi ya kidemokrasia kama Tanzania inaaminika kuwa kila kitu kinafanyika kwa utaratibu wa kisheria kupitia miongozo ya kikatiba kama sheria mama.

Kutokana na hilo kuna sheria znazomlinda rais wa nchi anapokuwa madaradakani hivyo kumfanya asiweze kufikishwa chin ya vyombo vya kisheria (mf. mahakama) pale anapokwenda kinyume na katiba (wanasheria mnaweza kunipa ufafanuz zaidi kuhusu kinga hiyo).

Swali ninalo jiuliza ni kwamba ni nini kitatokea endapo nchi kama TANZANIA, narudia tena nchi kama TANZANIA itapata rais asiye na vinasaba vya uzalendo na kuamua kuuza eneo la mkoa mmoja ulioko mpakani katika nchi hiyo jirani?

Mfano. Akauza eneo la mkoa wa mara nchini kenya au eneo lolote la mpakani.

Je, hili linawezekana?
-Sheria za nchi znasemaje?
-Sheria za kimataifa znasemaje?
-Jamii husika inaweza fanya nini, na umma wa watanzania unaweza fanya nini?

karibuni..!
 
Hilo haliwezi kutokea. Na iwapo jambo kama hilo litatokea basi huyo rais tutamuondoa asubuhi na mapema kwa mtutu wa bunduki kama tulivyomfanyia Nduli Idd Amin Dada miaka ile ya mwishoni mwa 70 alipoivamia ardhi yetu kule Kagera.
 
Kwanini lisiwezekane mbona watu wengi wamepotea na watu wake kimyaa tuu.Watu wasiojulikana na waliomshambulia Tindu Lissu mbona serikali iko kimyaa na inatuhumiwa?
 
Tate Mkuu hilo linawezekana maana ardhi ya mbuga ya Loliondo iliuzwa kwa mfalme wa falme za kiarabu na hakuna lolote ni kimya tuu!!
Inatakiwa katiba itakayodhibiti usalama wa nchi yetu sio hisani iwe sheri ya katiba!!
 
Hilo haliwezi kutokea. Na iwapo jambo kama hilo litatokea basi huyo rais tutamuondoa asubuhi na mapema kwa mtutu wa bunduki kama tulivyomfanyia Nduli Idd Amin Dada miaka ile ya mwishoni mwa 70 alipoivamia ardhi yetu kule Kagera.

Ulikuepo au unashadadia matango pori ya nyerere?
 
hatutaki maisha magumu kama yalivyosasa ..

ni kauli ya bibi yangu huku kijijini ..

MUNGU ANAWAONA
 
Hilo haliwezi kutokea. Na iwapo jambo kama hilo litatokea basi huyo rais tutamuondoa asubuhi na mapema kwa mtutu wa bunduki kama tulivyomfanyia Nduli Idd Amin Dada miaka ile ya mwishoni mwa 70 alipoivamia ardhi yetu kule Kagera.
Mtaweza au ndio kama maneno ya Roma mkatoliki?
"Leta wajedaaaaa, leta defenderrrr"
 
Hilo haliwezi kutokea hata awe dictator vipi sana sana watatekwa wananchi na sio kuuza kipande cha eneo kwa nchi jirani.
Kama idd amini mwenyew hakuiuza uganda bali alithubutu kuiongezea eneo kwa kuvamia eneo la mkoa wa kagera
 
Mtoa mada amesema ikitokea/wewe unasema haitatokea nadhani hapo bado hujamuelewa,kwani wewe ninani hadi ufahamu mawazo au malengo ya huyo Rais anayelengwa hapo?
 
Back
Top Bottom