Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,612
- 12,868
Nchi imezungukwa na maji kila upande,
Kuna mito, maziwa, na mabwawa ya kutosha, weka kando maji ya bahari halafu bado watu wanalia ukame.
Nchi iliyopo kwenye ukanda wa maziwa makuu kulalamika ukame siyo kituko hicho?
Maeneo mengi ya Tanzania yanapata mvua walau mara moja au mbili kwa mwaka.Badala watu wavune maji ya mvua na kuyahifadhi kwa ajili ya nyakati za shida, wanayaacha yanatiririka hovyo na kusababisha mafuriko.
Mafuriko yanasababisha uharibifu wa kila kitu halafu watu wanaanza kulia wasaidiwe, inakuwa mvua ikinyesha watu wanalalamika mafuriko, jua likiwaka watu wanalalamika ukame.Kwenye kila hali mtanzania ni mtu wa kulalamika tu.
Kitendo cha watu kulalamika pindi hali ya hewa inapobadilika ni hatari sana, maana hakimtofautishi binadamu na wanyama wengine sababu wote wana respond badala ya ku-react dhidi ya mabadiliko ya kimazingira.
Tatizo la ukame linakabilika kabisa kwa Tanzania, kama serikali, wananchi na wadau wengine wangeshirikiana tusingekuwa na stori za ukame wala njaa.
Serikali ingeweza kusambaza maji ya mito na maziwa kwenye maeneo yenye shida na kuwauzia wananchi kwa gharama nafuu.
Pia wananchi wanatakiwa kujitengenezea mabwawa madogo madogo kwa ajili ya kuhifadhi maji ya mvua pindi inyeshapo kwa matumizi ya baadae.
Tujitahidi kukabiliana na mabadiliko hasi ya mazingira na si kukubaliana nayo, ukame kwa Tanzania nayo ni aibu.