kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 20,142
- 24,444
Hivi sasa ndio katiba inachezewa kuliko kipindi cha uchaguzi!Uchaguzi umekwisha anashuhulika na maisha yake. Naamini akihitajika kisheria tutamuona au kumsikia.
Aliunguliwa au iliungulizwa?Kupitia vyombo vya habari tulisikia sliunguliwa hoteli yake.
Sasa sijui kaunguliwa mdomo au?
Kwa mtu anaejua na kuheshimu sheria hawezi tena kuhoji uhalali wa kisheria kwa rais alieapishwa,itakuwa anajipunguzia hadhi miongoni mwa wasomi wenzie,kazi kawaachia Sefu na LowassaBaada ya uchaguzi mkuu,aliibuka mwanasheria machachari alikuwa akichambua vifungu vya sheria na katiba ya nchi kwa utaalamu mwingi dhidi ya serikali ya ccm,lakini cha ajabu tangu uchaguzi wa marudio ufanyike na shein kupitia ccm kutangazwa mshindi huyu binti karume haonekani tena wala kusikika kwenye vyombo vya habari,
Wadau mwenye kufahamu alipo atujulishe na kwanini yupo kimya wakati mapambano bado yanaendelea!
Mwanasiasa wa msimu!Uchaguzi umeisha, amerudi kazini anaendelea na maisha yake, atarudi tena kwenye siasa kipindi cha uchaguzi 2020.
Siku ndio zinasogea hivyo!Alimpa Dr Shein miezi 6 ya kuongoza baada ya uchafuzi wa 25 March 2016. Alimuahidi Dr Shein private jet kama atavuka miezi sita ya uongozi wake. Yuko kwenye count down!
Baba yake mdogo Balozi Ali Karume ameteuliwa na Dr Shein kuwa Waziri wa mawasiliano. Lazima Fatuma aufyate sasa hivi. Na Serikali ya Zanzibar anaitambua!Baada ya uchaguzi mkuu, aliibuka mwanasheria machachari alikuwa akichambua vifungu vya sheria na katiba ya nchi kwa utaalamu mwingi dhidi ya serikali ya CCM. Lakini cha ajabu tangu uchaguzi wa marudio ufanyike na Shein kupitia CCM kutangazwa mshindi huyu binti Karume haonekani tena wala kusikika kwenye vyombo vya habari.
Wadau mwenye kufahamu alipo atujulishe na kwanini yupo kimya wakati mapambano bado yanaendelea!
Kiswahili kumbe bado haitoshi kuwa lugha namba moja TanzaniaAliunguliwa au iliungulizwa?
Ndio kipindi hiki tulihitaji mchango kuliko wakati wowote!CCM mnajipa moyo hapa tu, kinachoendelea Zanzibar na Kwenye ulingo wa siasa kimataifa najua mnatamaani kiwe ndoto na sio ukweli.
Sasa hivi mmefunga macho mkijiaminisha wakati wa kuyafungua moto utakuwa umezima, hauzimi!