Nini kimempata Shiza Ramadhani Kichuya?

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,238
Alianza kwa kasi ya mbwembwe ndani ya klabu ya Simba,hakujua kuwa kuna wale waliomtangulia walianza na mbwembwe na kushindwa....
Akitokea timu ya Mtibwa Sugar, katika mechi 13 za awali Ligi Kuu alifanikiwa kufunga magoli 9.

Ikumbukwe!
Alianza kwa kasi ya mbwembwe katika Ligi Kuu, baada ya kufumania nyavu mara tisa ndani ya michezo 13 pekee!

Mara ya mwisho winga huyu kufunga goli ni dhidi ya Stand United mwezi wa kumi na moja , mjini Shinyanga, akifunga goli lake kwa mkwaju wa penati.

Tangu mchezo huo imeshapita michezo 11 bila winga huyu kufumania nyavu za timu pinzani, michezo mitano ya Ligi Kuu Bara African Lyon, Tanzania Prisons, JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Ndanda FC hali kadhalika michezo 6 ya kombe la Mapinduzi KVZ, Taifa Jang'ombe, Jang'ombe Boys, URA, Yanga na Azam.

Michezo 11. Hii hijawahi kutokea kwa mchezaji yeyote yule wa Dar es salaam Young Africa SC, mara ya mwisho mfumania nyavu wa Mabingwa watetezi na wa kihistoria wa LigiKuu Bara kucheza mechi nyingi bila kusalimiana na nyavu ilikuwa mwaka 1983- ambapo mshambilizi hatari wa Yanga SC kipindi hiko ''Makumbi Juma'' alicheza michezo 8bila kusalimiana na nyavu.
 
Attachments

  • download.jpg
    download.jpg
    4.1 KB · Views: 147
  • 1.jpg
    1.jpg
    19.7 KB · Views: 167
Mshaanza kuwasakama sasa mmoja mmoja ...ni wachezaj wa simba tu ndo hua wanaonekana ...embu tafuten habar nyingine za kuandika ..achen ushabik maandazi
 
Ilikuwa nguvu ya Soda..sasa ni zamu ya wachezaji wa Azam kutesa..Mahundi kiboko wa Yanga aka Chura na Himidi Mao dawa ya Simba asiyeng'ata
 
Ilikuwa nguvu ya Soda..sasa ni zamu ya wachezaji wa Azam kutesa..Mahundi kiboko wa Yanga aka Chura na Himidi Mao dawa ya Simba asiyeng'ata
Nguvu ya soda ...nani anaongoza ligi kuu tanzania bara?? Mmeacha kusakama timu sasa mnaangalia mchezaj mmoja mmoja hahahhaa mwafaaaa
Endeeleen kujipa moyo watu wa azam na yanga 8G
mwafaaa
 
Mshaanza kuwasakama sasa mmoja mmoja ...ni wachezaj wa simba tu ndo hua wanaonekana ...embu tafuten habar nyingine za kuandika ..achen ushabik maandazi
Mkuu, mechi 11 si mcheo aisee...

ukizingatia ni mshambulizi tegemezi kwenye upachikaji mabao!
 
Ilikuwa nguvu ya Soda..
Mkuu, hapo kwenye ''NGUVU YA SODA'' nimekuelewa sana...

wachazeji wengi wa timu ile huwa ni nguvu ya soda....Alafu hawawezi kuishi na hype ya usupastaa.
yaani akibadilisha diet kuacha kula maandazi akaanza kula chapati ndipo huanza uchizi..
 
..sasa ni zamu ya wachezaji wa Azam kutesa..Mahundi kiboko wa Yanga aka Chura na Himidi Mao dawa ya Simba asiyeng'ata

Yaani unasema ni zamu ya azam kutesa wakati kwenye msimamo wa ligi wamepitwa zaidi ya alama 10..

sasa wanatesa nini hapo?
 
Nguvu ya soda ...nani anaongoza ligi kuu tanzania bara?? Mmeacha kusakama timu sasa mnaangalia mchezaj mmoja mmoja hahahhaa mwafaaaa
Endeeleen kujipa moyo watu wa azam na yanga 8G
mwafaaa
acha kuamini kuwa kuongoza ligi ndio kuwa bingwa...

nilikuthibitishia hili msimu uliopita.....ila bado hujajifunza.

mu mtegemeaye kwenye kutupia magoli ndio huyoooo..."AMESHA KATA UPEPO".
 
Nguvu ya soda ...nani anaongoza ligi kuu tanzania bara?? Mmeacha kusakama timu sasa mnaangalia mchezaj mmoja mmoja hahahhaa mwafaaaa
Endeeleen kujipa moyo watu wa azam na yanga 8G
mwafaaa

MKUU kweli mzima wewe?

mbona umeanza kupagawa. 8G ndio nini sasa?
 
acha kuamini kuwa kuongoza ligi ndio kuwa bingwa...

nilikuthibitishia hili msimu uliopita.....ila bado hujajifunza.

mu mtegemeaye kwenye kutupia magoli ndio huyoooo..."AMESHA KATA UPEPO".
Msimu wa tatu matopeni wanaanza vizuri lakini lazima wapotee mwishoni.
Imeishakuwa kawaida yao!
 
Hili nili viziaji lililo kubuhu, baada ya marefa kumshtukia tuu kwisha habari yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom