Nini kilitokea zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kilitokea zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmanga mswahili, May 29, 2012.

 1. m

  mmanga mswahili Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nini kilitokea zanzibar?
  kwa ujumla kumekua na haliya amani tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambo uliweka serekali y ashirikishi madarakani ukiachia changamoto ndogo ndogo za hapa na pale.
  kwa naman moja au nyengine MUUNGANO umekua na changamoto nyingi ambazo ni sawa na donda ndugu.
  tatizo ni kwamba propaganda zilizokua zikinadiwa na wapinzani wa ccm ambazo zinaukweli mdogo na chumvi nyingi na nyengine ambazo zimeshapatiwa ufumbuzi na kuwa si makero tena ya muungano bado zimekua vifuani mwa wapinga maendeleo na wanoumwa na muungano wetu uliodumu kwa miaka kadhaa sasa.
  mara baada ya kuwa na serekali ya shirikishi. wengi walitafuta nafasi ya kuexpose mawazo yao na kutaka waonekane ya kuwa wao ndio wanauchungu na visiwa vya zanzibar.
  miongoni mwao ni vikundi kama vinne vya dini ya kiislamu ambavyo viliungana pamoja na kujulikana JUMUIYA YA UAMSHO jumuiya yetu hio ndio iliomfunga paka kengele kwa kubeba bango katika kila kona ya nchi kwa kuhubiri kero hizo kwa maoni yao na wanavyohisi wao ambazo baadhi yake serekali ilishaolea ufafanuzi na nyengine ziko ziko katika pipe line ya kurekebishwa.
  na ndio wamefanikiwa kuwapata vijana ambao wanajazba kali na itikadi nzito za kiimani wakihusisha na vitu vyengine vya namna hio ambo wao sasa wamebeba bango na kufanya ni public agenda ambo iliteta vugu vugu ktk visiwa vya znz

  vipi limekuja hili?
  Hili limekuja baada ya serekali kuanzisha mchakato huu kwa kuanza matayarisho ya kuunda hadidu rejea na tume ya constituional review ambapo wale wanaopinga maendeleo walihofu kukamilika kwa mchakato huo na kuona ya kua adhma zao hazitokamilika ndio wakfanya intervention katikati kwa ahadi nzito na kutafuta sehemu ya kuliexpose kwa hoja ya kuwa kuwe na kura ya maoni kwanza juu ya huo MUUNGANO wenyewe na badala yake ndio maoni ya marekebisho yafuate baadae.

  kwa naman moja au nyengine serekali ya mapinduzi ilitumia muda mwingi kuona wanatoa maelekezo ya kuendesha mihadhara hio na kuwaomba vipi wafuate taratibu ili wawe katika njia sahihi.

  Tatizo ni nini?
  Tatizo ni HAMASA za vijana ambzo ziligusa katika hisia zao na itikadi zao kwa kuona ukimya ule wa serekali ni kutoweza kufanya lolote zidi yao na pia waliona wao ndio waamuzi wa kila kitu pia ukiachilia mbali muamko wa utaratibu wa sheria ambao kila mmoja weytu alipaswa kuuhashimu bila ya kushurutishwa.
  lakini baada ya kutoa taarifa ya kufanya mkutano vijana wakahamasika na kufanya maandamano ambayo walailazimika kupata kibali. nadio mana jeshi la polisi likamkamata kiongozi woa ili atoe maelezo ya nini kilifanyika wakati wao walitoa taarifa ya kufanya mkutano laikni mbona maandamano kulikoni.
  ndio vijana wakaamua kufanya hayo walioyafanya ambyo hadi sasa ni gumzo kubwa kubwa kwa visiwa na Tanzania kwa ujumla.
  ahsante
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ndo wachome makanisa!?
  kwakweli uchomaji wa makanisa umeniudhi sana!
   
 3. s

  silent lion JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mbona jamani nyie wabishi? Makanisa yamechomwa na infiltrators wanaodaiwa kutoka CCM ili kukipaka matope jumuiya ya Uamsho
   
 4. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Acha Makanisa, kuna taarifa zisizo tangazwa kuwa mali za Wabara kuchomwa pia hata nyumba zingine mkoa kazkazini zimechomwa
   
Loading...