Nini kilimuondoa Zamoyoni Mogella kutoka Simba kwenda Yanga

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
595
500
Miaka michache iliyopita Zamoyoni Mogella kipenzi cha wana-Simba alieleza kilichosababisha akaacha kuichezea Simba mwishoni mwa 1991. Anasema kwamba alichoshwa na vituko vya uongozi wa klabu hiyo na jinsi ilivyokuwa ikishindwa kuthamini wachezaji.

Sasa udadisi wangu umenirusisha nyuma kwenye historia ya wakati huo ili kuona mazingira yalikuwaje.

Kwanza Mogella alirejea na kuanza kuichezea tena Simba mwaka 1990, yeye na Hamis Gaga na mwaka huo Simba ikachukua ubingwa wa Bara. Mwanzoni mwa mwaka 1991, Simba ikaendelea kuwa hatari na hadi ikachukua ubingwa wa Kombe la Afrika Mashariki baada ya kuukosa kwa miaka 17. Mtakumbuka katika mashindano hayo Mogella akaibuka mfungaji bora.

Lakini mwisho mwa mwaka huo kwenye ligi Simba haikutetea ubingwa wa Bara na mechi ya mwisho ya Simba na Yanga, Simba ikaingia mitini kwa kuogopa kucheza na Yanga na Simba ikapoteza mchezo huo. Siku Simba inaingia mitini ilikuwa ni November 13, 1991 na nchicho kipindi cha mwishoni mwa mwaka.

Sasa Mogella anaposema kwamba uongozi ulikuwa ni mbovu na akaondoka kipindi hiki, basi ukiishia hapa kwa maelezo haya unaweza kuungana naye. Lakini hebu tuendelee mbele kidogo.

Tuendelee mbele kwa sababu kipindi hikihiki Simba iliweza kuifunga timu ngumu ya Pamba ya Mwanza mnamo November 5, 1991, goli lililofungwa na Hamis Gaga licha ya kukabwa vilivyo na George Masatu wa Pamba.

Lakini ni kipindi hiki ambapo Pamba iliingia kwenye ligi kubwa na kuifunga Malindi kwa penalty na kuchukua ubingwa wa Muungano. Hivyo Pamba ilikuwa ni nzuri na Simba ilikuwa ni nzuri.

Sasa tutaona kwa nini nimeiunganisha Pamba. Nimeiunganisha Pamba kwa sababu wakati Pamba inachukua ubingwa wa Muungano na Simba inapoteza ubingwa wa Bara basi maana yake ni kwamba Mogella akaondoka kipindi hiki.

Lakini tuendelee zaidi. Kuondoka kwa Mogella ambaye aliondoka na rafiki yake Hamis Gaga, Simba kipndi hichohicho yaani December 1991, Simba ikawasajili wachezaji wapya kutoka katika timu zifuatazo, yaani George Masatu (Pamba), Hussein Masha (Pamba), Mohamed Mwameja (Costal Union). Nimewataja wachache tu, lakini unaweza kuendelea ukawataja akina Fikir Magoso nk.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kumbe harakati za kuondoka kwa Mogella na Hamis Gaga ziliambatana na harakati za simba kuwaingiza hao wapya yaani Masatu, Masha, Mwameja na wenzao.

Wakati hao wapya wanakaribishwa Simba, Mogela na Gaga wakakaribishwa Yanga na hivyo mwaka 1992 umewakuta Zamoyoni Mogella na Hamis Gaga kama wachezaji wa Yanga!

Simba walikuwa ni moto wa kuotea mbali na Simba ikawa ni hatari zaidi. Kama mnakumbuka Simba hiyo ilienda Zanzibar na ikatetea kombe la Afrika Mashariki tena kwa fainali kali ya kuifunga Yanga kwa penalty ingawa katika zile penalties wote Mogella na Gaga waliifungia Yanga.

Sasa hapa cha kujiuliza ni kimoja. Kama uongozi ulikuwa ni mbaya na haujali wachezaji, ilikuwaje uongozi huo walioukimbia akina Mogella uchukue wachezaji wazuri zaidi kutoka kwenye timu bora yaani Pamba. Kuchukua mchezaji yeyote kutoka Pamba ilikuwa ni kazi nzito, sasa hapa wakachukuliwa wa kutumainiwa yaani Centre-Half, Masha na namba 4 yaani George Masatu, ingawa alipokuja Simba alibadili namba na kuwa Centre Half.

Narudia tena, kama suala lilikuwa ni uongozi, iweje uongozi huo ufanikiwe ku-replace akina Mogella na timu bora zaidi.

MImi nashawishika kudhani kwamba kuna sababu nyingine huenda wadau mnaijua. Saidia kufafanua nikijua JF ni kisima cha uchambuzi
 

Rockcity native

JF-Expert Member
Dec 31, 2012
2,138
2,000
kuhama tim zipo sababu nyingi tu japo mtu anaweza kutumia sababu moja kama kichaka cha kuficha sababu nyingine... hata lunyamila alikua kipenzi cha wanayanga lakin alienda simba pasipo mtu yoyote kutegemea,, hivyo hivyo kwa mohamed hussein 'mmachinga'.... mwisho wa siku sababu ya kiuchumi ndo kubwa inayomfanya mtu kuhama licha ya mpira wa zamani kujaa mapenzi ya tim kuliko pesa..
 

Kitumbikwela

Senior Member
Nov 5, 2016
140
225
Kuondoka kwa Mogella kipindi hicho kwenda Yanga hakuna tofauti na jinsi Simba walivyomuachia Tambwe kwenda Yanga kwa sababu ambazo mpaka leo ukiwauliza watu wa Simba wenyewe wanashindwa kuzielezea vizuri.
Imekuwa ni kawaida kwa Simba kuwaacha wachezaji wenye mchango kwenye timu halafu wanashindwa kupata substitute wa uhakika, mfano mpaka leo Simba wana tatizo la striker wa uhakika ingawa wanashinda kupitia viungo.
 

naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,687
2,000
Mogela alikua mmoja ya wachezaji wa zaman waliojali maslah sana na ndio maana ni mmoja kati ya wachezaji wa zaman wanaoishi vizur mtaani;Kuchukuliwa akina Marsha haina maana kuwa viongozi walikua wanajali wachezaji wote. Viongozi wa timu kubwa na wafadhili wa wakati ule walikua na wachezaji wao wanaowathamini wakikohoa tu wanapewa mzigo,Mogela alikua ndio anaishia kwenye mpira kipindi anaenda Yanga na Gaga inasemekana alipiga mpunga mrefu kutoka kwa Gulamali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom