Nini kilichosababisha kifo cha mchezaji wa Simba, Hussein Tindwa?

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
12,902
15,330
Bado kuna utata kuhusu kilichomsibu aliyekuwa beki wa klabu ya soka ya Simba Sports Club marehemu Hussein Tindwa aliyefariki dunia walipokuwa wakicheza na timu ya Racca Rovers ya Nigeria.

Hiyo ilikua ni ktk kinyang'anyiro cha mashindano ya kutafuta klabu bingwa barani Afrika mwezi Mei mwaka 1979 ktk iliyokuwa uwanja wa taifa leo hii ukiitwa uwanja wa Uhuru.

Endelea kusoma kwenye link hapa chini.

=======
1698000179946.png
WIKI iliyopita tulilitambua jina halisi la mchezaji Hussein Tindwa aliyefia uwanjani mwaka 1979, wakati akiitumia Simba katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam (sasa Uwanja wa Uhuru).

Tuliona jinsi mchezaji huyo alivyobadilishwa jina lake halali la Hassan Tindwa na kuitwa Hussein Tindwa ambalo ndilo kila mtu analifahamu hadi leo hii.

Kifo cha mchezaji kilitikisa nchi kilitokea Mei 12, 1979 wakati Simba ilipokuwa ikicheza dhidi ya Racca Rover ya Nigeria katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika (sasa Ligi ya Mabingwa Afrika). Kabla ya mchezo huo, Simba ilitoka kuitoa Mufulira Wanderers ya Zambia kwa idadi ya mabao 5-4. Ilifungwa 0-4 na kwenda kushinda Lusaka 0-5.

UTATA WA KIFO CHA TINDWA
Kuna maneno mengi sana yalizuka baada ya kifo cha mchezaji huyo, kila mtu alikuwa akizungumza lake.
Beki huyo wa kati, ndio kwanza alikuwa ameanza kuaminiwa, alipoteza maisha uwanjani na tukio hilo kwa kiasi kikubwa lilihusishwa na imani za ushirikina.

Katika tukio hilo, Tindwa aliruka juu na mchezaji mmoja wa Racca Rovers, kuupiga kichwa mpira wa krosi kuondoka hatari langoni mwake, mara baada ya kucheza mpira huo, alidondoka chini hakuinuka tena.
Mwamuzi wa mchezo, alipuliza kipyenga kusimamisha mchezo ili kumwangalia alikuwa amepatwa na masahibu gani. Tindwa alikutwa akiwa amepoteza fahamu inadaiwa damu zilikuwa zikimtoka masikioni, puani na mdomoni.

Mchezaji wa kwanza wa Simba kufika eneo la tukio, alikuwa ni Mohamed Kajole (naye marehemu kwa sasa). Katika fikra zake, Kajole alidhani Tindwa alikuwa amepoteza fahamu tu.

WACHEZAJI WALIFICHWA
Tukio hilo lilitokea katika dakikia za mwisho kufikia mapumziko. Tindwa alitolewa uwanjani kwa kubebwa na machela na baada ya kuonekana tatizo lake lilikuwa kubwa, aliingizwa kwenye gari la wagonjwa kupelekwa hospitali.

Wapo wanaosema Tindwa alifariki dunia palepale uwanjani, pamoja na jitihada zilizofanywa za kupekwa hospitali.

Wengine walidai alifariki wakati akiwa njiani na wengine wakidai alifia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Taarifa za kifo chake zilipatikana kabla ya mchezo haujaisha lakini wachezaji wa Simba walifishwa.

MANENO YA MTAANI SASA
Labda kutokana na kutokwa na damu katika mwili wake, baadhi ya watu walidai tukio hilo lilitokana na ushirikina.

Kingine kilichochangia imani hizo ni kitendo cha Tindwa kuonekana akiwa uwanjani alipokuwa akimwonesha kidole kipa wale Mambosasa.

Inadaiwa Simba iliweka kambi yake Africana Hotel (wengine wanadai kambi ilikuwa Njuweni Hoteli, Kibaha) na katika kujiandaa na mchezo huo, ilimleta nchini mganga kutoka Mombasa, Kenya.

Inadaiwa mganga huyo alimkabidhi Tindwa hirizi kwa ajili ya kuweza kusaka ushindi katika mchezo huo.
Kuna kiongozi mmoja wa Simba (jina ninalo) aliwahi kuniambia Tindwa alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji waliolala katika makaburi ya Mburahati jijini Dar es Salaam siku moja kabla ya mechi kwa ajili ya kusaka ushindi wa mchezo huo.

Wanaoamini mambo hayo wanasema, mganga wa Simba alizidiwa na ndumba za Racca Rovers na kusababisha kifo cha Tindwa.

MADAI YA RUSHWA
Madai mengine yalikuhusu rushwa na ushirikina kwa pamoja. Inadaiwa wachezaji watatu, Athuman Mambosasa, Firbet Rubilira na Tindwa walidaiwa kupokea rushwa kutoka ubalozi wa Nigeria, Barabara ya Bagamoyo (sasa Ali Hassan Mwinyi).

Baada ya tuhuma hizo alitafutwa mganga kutoka Bagamoyo kwa ajili ya kusoma Halalibadili kwa ajili ya wachezaji. Wapo wanaomini hicho ndicho kilichoyaondoa maisha ya Tindwa.

SABABU ZA KITAALAMU
Hata hivyo, taarifa za kitaalamu zinasema Tindwa alikuwa na matatizo katika moyo wake. Inadakiwa alikuwa na moyo mkubwa ambao usingeweza kumfanya acheze soka.

Ilifikia hatua, madaktari walijiuliza mchezaji huyo aliwezaje kumudu kucheza soka kutokana na hali hiyo. Kutokana na madai hayo inadaiwa moyo wake ulihifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

MATUKIO MENGINE
Mchezani wa kimataifa wa Nigeria, Nwankwo Kanu alizaliwa na kasoro ya moyo ya kuzaliwa, aligunduliwa na kufanyiwa upasuaji mwaka 1996.

Pia, katika Kombe la Mabara, uwanjani, Gerland, Lyon Juni 26, 2003, mchezaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon, Marc Vivien Foe akicheza dhidi ya Columbia dakika ya 72 alianguka na kufariki dunia.

Mchezaji wa Bolton, Fabrice Muamba Machi 17 2012, katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA kati ya Bolton dhidi ya Tottenham Hotspur uwanjani White Hart Lane, moyo wake ulisimama kwa dakika 78.

Muamba alianguka uwanjani baada ya kupatwa na mshtuko akiwa uwanjani, aliwekwa chini ya uangalizi maalumu na aliachana na soka kabisa.
 
Kongole kwa picha,nawaona kwa mbali ninawowakumbuka Martin Kikwa,Abdallah Mwinyimkuu, Mohamed Bakari Tall, Mohamed Kajole,Willy Mwajibe,ila vijana wa zamani, Nywele zilikua nyingi mno,ila sasa hv vipara vimetawala doo!!Mabugaloo na Raizon ngazi mbili mpaka tatu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom