JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,966
Wadau poleni ni mihangaiko, leo nataka tutafakari hili jambo kwa pamoja, ni nini hasa kiini cha maumivu ya kimapenzi? Kwa nini ukiachwa na mpenzi hasa unayempenda maumivu huwa makali? Kwa nini ukimfumania mpenzi wako maumivu huwa makali? Mbaya zaidi hata kwa mpenzi uliyemwacha mwenyewe siku ukimuona anatoka guest na mtu wake bado unaumia. Kwa nini iwe hivi kana kwamba hakuna watu wengine utapata? Kituko ni kwamba, wewe ukiwa unachepuka husikii maumivu yoyote hata kama unajua unayechupuka naye siyo mtu wako na unajua ana mtu wake wala husikii wivu wowote.
Kwa upande wangu kiini cha tatizo hili ni ubinafsi tu wa watu, maana hakuna sababu nyingine ambayo huwa inaniingia kichwani maana nyingi zina majibu, wanawake ni wengi tena wazuri kuliko huyo na wanaume ni wengi tu wenye kukuhitaji kwa nini sasa uumie??
Karibuni.