Nini kifanyike kunusuru mpira wetu Tanzania?

moodykabwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
625
602
Taifa Stars.jpg

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Starts

Naomba tujadili wataalamu wa mpira..

Ni kwanini mpira wetu Tanzania umegubikwa na maneno maneno sana? Nini kifanyike tutoke hapa Tulipo??

Nawasilisha kwenu wazalendo wa Tanzania.
 
1.Tuache uchawi,majungu,ujuaji mwingi.
2.Tuwe na timu za vijana na watoto na ziendelezwe.
3.Serikali ichukulie soka kama biashara nyingine na itoe full support kwa vilabu.
4.Tutengeneze makocha wa kutosha.
 
1. Malinzi aondoke pale TFF
2. Soka la Vijana litiliwe mkazo
3. Mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA yapewe kipaumbele
4. Mashindano ya Kombe la Taifa yarejeshwe
5. Kozi za Urefa na Ukocha zitiliwe mkazo kuanzia shule za sekondari
6. Kuhakikisha viongozi wa Vilabu na vyama vya soka wanafanya uchaguzi kwa mujibu wa Katiba
7. Zifunguliwe Academy za kufundisha wachezaji
 
Kikubwa na cha muhimu ni TFF kuandaa mipango ya maendeleo na serikali yetu kutoa support ya kutosha kwenye maendeleo hayo, hamna nchi inaweza kuendelea kisoka bila serikali kuhusika.

Kwa hapa kwetu sijaona kama serikali yetu inasupport mpira.
 
1. Serikali itambue rasmi kuwa michezo ni fani kama zilivyo nyingine kama udaktari, uhasibu nk
2. Baada ya kutambua michezo kama fani nyingine, ipewe nafasi na wataalamu wa kutosha toka shule za awali.
3. Serikali iweke mkazo kwny michezo kwani ni chanzo kikubwa cha mapato na ajira kwa vijana. Michezo inaweza kuajiri vijana wengi ambao hawana ajira kama fani nyingine nyingi.
4. Nguvu iongezwe kwa soka la watoto na vijana.
5. Mifumo ya uongozi katika taasisi zinazosimamia ni mbovu sana.
6. Malinzi na TFF wajiuzulu, wamefeli jumla
 
Naomba tujadili wataalam wa mpira ni kwann mpira wetu Tanzania umegubikwa na maneno maneno sana??

Nini kifanyike tutoke hapa Tulipo??

Nawasilisha kwenu wazalendo wa TANZANIA
TFF ivunjwe. Kama alivyofanya JK kumpata Maximo, tuende nchi za ulaya mf. Ufaransa tukaombe wazee wastaafu waliopata kuongoza soka nchini mwao. Waje waongoze TFF huku wakituwekea misingi mizuri. Wachawi wa soka laTz si TFF bali ni vilabu vitatu, Yanga na Simba vyenye dhambi ya kuweka mawakala wao hapo TFF badala ya viongozi, na Azam inayotumia nguvu ya pesa ku-influence maamuzi mbalimbali.

Tunahitaji tupate watu neutral wasiojua Simba wala Yanga bali kanuni za soka, watujengee misingi thabiti.
 
MALIPO
Baadhi ya wachezaji ligi daraja la nne na la pili wanacheza kwa kujitolea tu hawalipwi na wakilipwa wanapewa shs 10,000 mpk 15,000 kwa mechi wakiumia hakuna huduma za matibabu wanakwenda kutibiwa na familia zao.

Baadhi ya timu ligi kuu wachezaji wanalipwa 300,000 chini ya laki5 na bado wanacheleweshwa kulipwa..mchezaji yupo uwanjani anakuwa na stress kibao, familia itakula nn, kodi atalipa vp, ada ya shule kwa mtoto, ataweka akiba vp ajenge nyumba nk

Ifikie hatua michezo ipewe thamani na mpira uwe unalipa angalau na sisi tusikie mchezaji kanunuliwa japo milioni 100 kwenye club angalau watu wapate hamasa waongeze juhudi mpira unalipa.

Ifikie hatua mchezaji ligi kuu alipwe japo milioni 30 kwa mwezi na standards kiwango cha chini alipwe japo milion 3-5 after tax
 
Taarifa: wachezaji wanaolipwa hiyo mil 3-5 wapo japo wengi ni wakigeni.
 
Wachezaji wa kigeni tusajili walio na umri mdogo,TFF ivunjwe,waajiriwe watu waliosomea mpira.Mapato viwanjani yasimamiwe na serikali.
 
Tuwe na wachezaji wenye maumbo makubwa"The Giants"otherwise tutawasindikiza sana wengine.Maximo alitaka kutafuta vijana wenye miili nyumba wasio na nia njema wakampinga.Wachezaji wetu hawana utimilifu wa miili hata aje Sir Alex tutamfukuza
 
Miundombinu kama viwanja vya kisasa ,uweke watu wa mpira kabisa wenye action tu na sio maneno 2; weka academy kila mkoa na ziwe na wataalamu haswa waliobobea kwenye masuala ya academy 3; Weka team ya scouting ya kutosha nchi nzima ili kubaini talent za wachezaji.
 
Nimejaribu kufwatili katiba za vilabu mblai mbali za ligi kuu Tanzania kiukweli hakuna katiba ilioko kwa ajili ya mpira

Hizi Timu zote zipo kwa ajili ya kisiasa tu Watu waje watengeneze majina yao uchaguzi ukifika utasikia wanagombea ubunge au udiwani
 
Nikimkumbuka Imani Madega naanza kuuona ukweli ktk hoja yako.
 
Nikimkumbuka Imani Madega naanza kuuona ukweli ktk hoja yako.
Pia bwana Rage
Pia manji ni Diwani
Pia manyama mjumbe wa kamati tendaji ya Yanga ni Diwani

Pata picha viongozi wengine waliobakia ni viongozi wa vyama vya siasa
 
Back
Top Bottom