Kamarade,
Ili Maoni haya uliyoyaita "maoni yangu", ambayo ni uthibitisho kuwa hayakufanyiwa utafiti, nadhani ushauri wako ungelikuwa na nguvu na uzito mkubwa kama ungeliungana na uthibitisho wa takwimu.
Kwa mkono wako umethibitisha pia kuwa "mimi binafsi ninawajua wapiga kura wengi", uwingi ni relative. Hujatuambia wapiga kura hao ni wa chama gani, age group gani, eneo gani. Takwimu za namna hii ndio ingelituonyesha usahihi na uimara wa maoni yako ili tushawishike kuyapokea na kuyatekeleza yote au baadhi yake.
Hoja ya Katiba, na ya kuungana kwa vyama, kwa mimi niliyefika Wilaya zote za Tanzania, ninaielewa matatizo yake kwa Watanzania wa kawaida. Mtu ambaye anakimbilia kikombe cha chumvi kuuza haki yake ya kura sidhani kama anaona umuhimu wa "Katiba" katika maisha yake.
Tunahitaji kuwasaidia kwa kutoa elimu, na kwa hali ya sasa ni lazima lugha zetu zishuke kutoa elimu ya uhusiano wa Katiba na maisha yao. Lakini huu si wakati wa kuzungumzia tena mabadiliko ya kawaida, kwa kuwa kama unafahamu mchakato wa kubadilisha Katiba, basi saa hizi ungelitupa ushauri bora zaid kuliko wa Katiba.
Kama kwa bahati mbaya hufahamu, basi ni vema nikakueleza tu kuwa ajenda hiyo kwa sasa haiwezekani, haina tija, na kwa wananchi wengi wakati wa Kampeni ni sawa na kuwaeleza maisha mazuri ya Washingtone, yaani japo kweli marekani ina maisha mazuri, lakini wanachohitaji watanzania wengi ni namna gani watatoka katika hali ya sasa.
Hivyo ajenda yeyote, itakayowapa matumaini ya haraka kutoka hapa walipo itakuwa ndio ajenda zenye tija. Kuhusu vyama kuungana, nadhani niliisha kutoa elimu ya kutosha katika Forum hii sina sababu ya kuirudia. Msimamo wa Chadema ni pale panapokuwa na Chama Makini na serious cha kuungana nacho, basi tutaungana nao.
Lakini tumeisha kujeruhiwa sana, na nadhani sisi tuliojeruhiwa ndio tunaoelewa maana ya kujeruhiwa, kuliko mtu mwingine yeyote anayetazama kutoka nje.Pamoja na hayo tunashukuru sana kwa maoni yako, inatusaidia kuwa focused zaidi.