Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
Nini hatima ya Korosho msimu ujao..
Ni swali dogo lakini majibu yake ni magumu.
Hofu imetawala kwa wafanyabiashara na wakulima na wadau wengine kuhusu hatima zao za malipo na kilimo cha msimu ujao.
Halmashauri zilizokuwa zinategemea levy za korosho kama chanzo cha mapato ya ndani zipi kwenye sintofahamu juu ya kiasi walichotegemea ambacho wakishakiingiza kwmatika mipango na bajeti zao za 2018/19.
Vyama vya msingi vya ushirika ambavyo ni wasimamizi na wasambazaji wakuu wa pembejeo kwa wakulima ikiwemo madawa nk havijui vitarejesha vipi gharama walizoingia kwa kukopesha pembejeo kwa wakulima wao.
Kwa mtazamo mdogo ni kuwa season ijayo itapata mtikisiko mkubwa.
Mtikisiko utatikisa Halmashauri kimapato..
Vyama vya ushirika kwenye mipango yao na madeni ya suppliers...
Wakulima hatima za mazao yao kwani wasiwasi wa kupata pembejeo na nyenzo nyingine....
Wafanyabiashara wa kati nao ambao ndio oxygen ya wakulima hawana hakika na walichotumia kukirejesha baada ya kukosa uhakika wa kulipwa kwa kukosa uhakiki wa mashamba.
Ni vigumu kwa wakulima(wamiliki wa mikorosho) kuweza kuhimili mikiki ya kuhudumia mikorosho kwa kuipa matunzo,dawa,palizi,ulinzi.,mavuno,uokotaji,ununuzi wa viroba,gharama ya kusafirisha kutoka shambani hadi kwenye vyama vya ushirika,tozo za vijiji tozo za masoko/halmashauri.......
Hekaheka ambazo wakulima huwaachia wafanyabiashara/ madalali kurisk na kusubiri kwani wao hawana mitaji na pumzi ya kusubiri malipo ya minada yanayochelewa ilhali wao wana mambo mengi yanahitaji utatuzi wa kifedha hivyo WAKOMBOZI wao huwa ni wafanyabiashara ambao kwa sasa hawajui kama mwakani watakuwepo.
Kibaya zaidi ni upande wa soko...soko huendana na wakati na hitaji(demand)
Hitajio huenda na ubora wa zao(fresh product) na mipango ya wanunuzi
Hivyo vyote kwa upamoja wake vikivurugika soko huanguka na huwa ni one way merchandise ambayo muuzaji humpigia magoti mnunuzi na mnunuzi huamua bei aitakayo....
Kwa kifupi hatima ya Korosho kwa msimu ujao ni kizungumkuti...
Korosho haina Baba(Bodi imevunjwa)
Haina mama(Vyama vya msingi)
Haina wadau(Wafanyabiashara)
Na haina walezi(Wakulima)
Tutegemee muanguko!!
Bisha ujifurahishe