Nini faida ya ushirikina na uchawi?

Nini faida ya ushirikina na uchawi?

Doyyi

Member
Joined
Mar 9, 2014
Posts
61
Reaction score
36
Tabia ya uchawi na ushirikina inazidi kuongezeka hasa mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na Shinyanga, huko Nkome GEITA walimu wameikimbia shule kwa kuteswa na wachawi.Hivi wenye tabia hizi wanafaidi nn zaidi ya kumkosea MUNGU?
 
Hakuna faida zaidi maisha ya mashaka na kubaki maskini ktk maisha yako yote
 
Shetani kakamata, kama vile ushoga, uzinzi, uongo, wizi n.k vyote havina faida zaidi ya madhara.
 
Yote mabaya uyajuayo hapa chini ya jua nyuma yake iko nguvu kubwa ya ushirikina na uchawi, dhumuni kubwa ni kumtesa binadamu kwa kila hali.
 
Havina faida mateso duniani na baada kufa roho ya mtu inakwenda jehanamu(motoni milele).
 
Hakuna faida zaidi ya umasikini maishani. Mashaka makuu juu ya kifo chake mchawi maana anajijua kabisa akifa ni motoni milele na milele. Wengine wanatamani kuacha lakini wanashindwa kwasababu ya mikataba ambayo tayari wameingia na majini vibaraka vya shetani. Kuacha ni mpaka Yesu mwenyewe aingilie kati na kukupa ulinzi wake
 
Hakuna faida yoyote zaidi ya kujizidishia umaskini tu na maisha ya mashaka...
 
Back
Top Bottom