Nini faida ya kumiliki website au blog?

mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,567
6,409
Wakuu habari za jioni,

Kama heading inavojieleza hapo juu,

Naomba kujua ni jinsi gani wamiliki wa website na blogs wanavopata faida kutoka katika blogs na website, mfano 1. Millardiayo 2. JamiiForums.
 
kipato kupitia matangazo hapa wadhamini ndio wadau
pia kama unataka kujulikana tu
 
MAPATO YA WEBSITE HUTOKANA NA MATANGAZO KWA MFANO APA JAMII FORUM UNAEZA ONA MATANGAZO YA VODA NA MENGI NEYO, WANALIPWA KUWEKA IZO MATANGAZO!
 
Ukitaka utengeneze pesa nzuri kwenye blog usifanye blog yako kuwa biashara bali fanya biashara yako kuwa blog.

Ninachomaanisha hapa ni fikiria unataka kutoa bidhaa au huduma gani kwenye soko (biashara) ikisha tengeneza blog kuwafikia watu wako, kuwaelimisha na kujenga uaminifu, ikisha hakikisha una smaku ya mtandao (online marketing system) itakayokusaidia kukufanyia mauzo.

Ukifanya blog kuwa biashara yako utahitaji
  1. Traffic kubwa sana
  2. Kutegemea mapato kutokana na matangazo
Traffic itakugharimu muda na/au hela na hasara ya matangazo ni kuwa inawaondoa watu waliofika katika tovuti yako na kuwapeleka kwenye tovuti ya wenzako badala ya kuwatumia watu hao kukuzalishia pesa.

Na ndio maana ma bloggers kama Neil Patel na John Morrow waliotengeneza mamilioni ya dola kwenye blog zao hawaweki matangazo kwenye blog zao kwani wale watu ni asset kubwa kuliko matangazo.
 
Kwa iyo wanavyofungua watu unapataje pesa mfano wamefungua watu 300 kwa siku
 
Kwa iyo wanavyofungua watu unapataje pesa mfano wamefungua watu 300 kwa siku

Ukitaka kupata pesa nyingi kwenye blog, usiendeshe blogu kama blogu.

Endesha blogu kama mfanyabiashara.

Mfanyabiashara anakuwa anatoa bidhaa/huduma yenye ku-solve matatizo ya watu fulani.

Tumia blogu kuelisha watu kuhusu matatatizo yao na waonyeshe suluhisha na tumia blog hiyo kuweza kuuza bidhaa au huduma unazotoa.

Hiyo ndio formula yenye kuingiza pesa nzuri kwenye blogu kuliko formula nyengine yoyote.
 
Good

Kwahiyo mkuu,

Baada ya kuwaelimisha watu na matatizo yao let say, hiyo blog ikawa na visitors wengi, then utumie mwanya huo kuwauzia hao visitors bidhaa yako ?

Mbn inakuwa ni kama tu mtu anayetafuta wateja kupitia Instagram account yake kuwa na followers wengi, kuna u tofauti gani hapo? Au mm ndio sijakuelewa..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaotumia Instagram wengi wao hawablog bali wana promote bidhaa zao moja kwa moja.

Kosa kubwa sana.

Chukulia mfano wewe unafanya biashara ya kuwatengenezea watu website.

Unatumia blogu yako:
  1. Kuelimisha watu kuhusu jambo lolote litakalowanufaisha wateja wako watarajiwa kuhusiana na topic ya website k.m. "Jinsi ya kutumia tovuti yako kutengeneza Tshs. 1,250,000 kila mwezi" au "Mambo 5 ya kuelewa kabla ya kumtafuta web designer" au "Maswali 5 ya kumuuliza web designer kupima ujuzi wake."
  2. Kukusanya taarifa zao (majina na email) kwa kutumia smaku ya mtandao (nimeongelea kiundani topic hii hapa).
  3. Kujenga mahusiano ya karibu kwa kupitia email marketing
  4. Kutoa ofa za bidhaa/huduma unazotoa.
Kwa hivyo unatumia blogu kama mlango wa kuwakaribisha wateja wako watarajiwa katika dunia yako kabla ya ku promote chochote kwao.

Unaji position kama mtaalamu na sio kama mmachinga.

Na unatumia smaku ya mtandao (online marketing system) iliyounganishwa katika blogu yako kujenga mahusiano mazuri zaidi na wateja wako watarajiwa na kuuza bidhaa au huduma unayotoa.
 
Hebu tuangalie faida zitokanazo na kuwa na wavuti ya kampuni;
reach-more-peoplez_881c9.jpg

1. Kuwafikia watu wengi zaidi.

Kama tulivyoona, kwenye watu kumi, mmoja anatumia internet, je hutaki kuwa wa kwanza kumshawishi huyo mtu mmoja atumia biashara yako? Kwa kuwa na wavuti utawafikia sio tu wale walio karibu yako, balo pia hata watu walio maili elfu na elfu.
2. Kuvutia wateja makini
Chukulia mfano wewe una duka la nguo, wateja wengi wangependa kupata taarifa juu ya mzigo mpya, mapunguzo nk bila hata kuja dukani kwako. Kwa kuwa na wavuti, ni dhahiri utavutia sana wateja makini ambao hupenda kupata taarifa za kina kabla ya kununua bidhaa. Wavuti inakupa wasaa wa kujieleza kwa undani juu ya huduma au bidhaa zako.
3. Kujenga uhusiano wa karibu na wateja.
Je umewahi kujiuliza, ni wateja wangapi ambao huwa marafiki zako baada ya kutumia / kununua bidhaa yako? Je unatumia njia zipi kudumisha uhusiano kati ya mteja na mtoa huduma? Wanazuoni husema, biashara itakayodumu ni ile tu iliyofanikiwa kujenga uhusiano mzuri na wateja wake. Kwa kuwa na wavuti, sio tu utaweza kupata maejesho juu ya ubora wa huduma yako, bali pia utaweza kudumisha mawasiliano kati yako na mteja, kumbuka mawasiliano ndio hudumisha uhusiano.
4. Kufanya biashara moja kwa moja.
Katika dokezo lango moja kwenye Facebook, niliwahi kuandika " Goodbye IT, welcome Digital Business", wengi hawkuelewa nini nilimaanisha hadi pale nilipokuja kufafanua, na kuna waliochanganya na hii huu mfumo wa digitali. Kwenye makala hii niliposema Digital Business nilimaanisha kutumia IT kama biashara ndio tunachokiita digital business.
Ukweli ni kuwa, Watanzania wengi wamekuwa wagumu na bado hawaamini kama kuna uwezekano wa kufanya biashara moja kwa moja online. Hii inawezekana ni kutokana na kasumba yetu ya kuogopa kuanza hadi pale tunapoona mtu amefanikiwa.
Ukweli ni kwamba, tunaweza kuuza na kununua moja kwa moja online, tena ukizingatia Tanzana ni nchi yenye watumiaji wengi wa simu za mkononi ambazo pia huwawezesha watu kulipia kwa kuhamisha pesa. Hivyo kwa kutumia huduma hizi, unaweza kufanya bishara moja kwa moja. Chukulia mfano wamiliki wa migahawa, maduka ya urembo nk. Wavuti inaweza kuwasaidia watu hawa kupanua na kuboresha wigo wa huduma zao.

www.muzecom.com
 
Back
Top Bottom