Nini faida ya kulipa kodi hapa nchini?

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,184
259
Wana Ukumbi, salam kwenu, mm ni mtz mjasiriamali mdogo sana, infact ndo naanza ujasiri. Nina maono ya kuikuza biashara yangu na kuwa ya kubwa. Sasa, naomba mnijuze, nini faida ya kujisajili na TIN na kuwa mlipakodi katika hatua hz za mwanzo. Kuna ulazima wowote kwa sasa? Ndugu asanteni sana na barikiwa sana!
 
Dah jamani ee! Mbona hv? Kimyaa! Tafadhali nahitaji elimu
 
VAT inalipwa baada ya kufikia mauzo fulani, kama biashara inauwezo wa kuuza million 40 kwa miezi 12, kisheria mtu huyu anapashwa kulipa kodi. Na atakiwa kujisajili kwa kutumi TIN namba aliyopewa. Lakini yote haya yatategemea kama umetunza hesabu za mauzo (book keeping) ili rekodi hizo ziweze kufanyiwa assessment of income.
Hebu ni PM niweze kukusaidia. Kwa sababu hiyo ni kazi ya mhasibu, na kukuelezea inaweza kuwa maelezo marefu ambayo yatakuchanganya tu.
 
Achana na kodi maana sioni haja ya kuwa mzalendo, ...... tunaambiwa kwenye madini hakuna kodi inayotozwa na ikitozwa haizidi 4% -5%., sasa kweli tutafika!!?
 
Back
Top Bottom