Nini Faida ya Jeshi la Polisi kwa Zanzibar na wazanzibari

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Wananchi wa Zanzibar ambao wamekuwa wakipatikana na mambo ya maajabu kila unapokaribia uchaguzi,wakati wa uchaguzi na baada ya Uchaguzi.

Suali kwa na utumwa kwa Wabunge wa Zanzibar ambao wanashiriki katika vikao vya Bunge mbali mbali kwa nyakati tofauti ndani ya miongo ya kila mwaka.

WaZanzibari wanashuhudia vitendo vya uvunjifu wa hali ya amani kwa kuvamiwa na magenge wanapigwa na kuumizwa na hata kuuliwa au kuachwa na vilema na makovu yanayotisha ,kwa kupigwa ama kwa kutumia nondo,minyororo au vitu vyenye ncha kali ,hayo huwakuta watu wa aina zote kwa maana weusi na weupe iwe wapo CCM au CUF ,kwani vijana wanapokusanyika huwepo mchanganyiko wa watu wote,ila ukweli wanaovamiwa na kulengwa na wananchi wanaoshabikia vyama vya upunzani.

Ajabu ni kwamba na inasemekana magenge hayo yanajulikana ,kutoa taarifa au kuarifu ni akina nani wanaofanya vitendo hivyo kwa mwananchi ni jambo la hiari kwani kazi ya upelelezi na wapelelezi ni kazi ya vyombo vya serikali.

Kufupisha genge la hivi karibuni likijulikana kama mazombi na hawa huvaa sare za utesaji kwa maana ya kuvaa soksi au kofia zinazoficha sura wanapoenda kuwashughulikia wananchi wasio na hatia.

Habari zao Waziri wa Ulinzi anazijua,Mkuu wa polisi anazijua,Mkuu wa jeshi anazijua,Waziri Mkuu anazijua na kama haitoshi Raisi anazijua.

Kwa upande wa Tanganyika ambayo ni sehemu ya nchi mbili zinazounda Muungano kulizuka PANYA genge ambalo lilitikisa Dar .Police Dar hawakusita kulipeleleza na kusikika na kuonekana kwenye vyombo vya habari kuhakikisha wanawatia hatiani na kweli walipambana na si kupambana waliwakamata na kuwasambaratisha leo kundi hilo halipo,

huku upande mwengine wa Muungano ambako ni Zanzibar hakukusikika mkuu wa polisi wala upelelezi wake wala afande kuwahakikishia wananchi kuwa watawatafuta na kuwasaka ili kuhakikisha wahusika wanafikishwa mahakamani na genge hilo kuangamizwa

Inasemwa ulinzi ni jambo la Muungano ,Waziri atueleze alihakikisha vipi wahusika wanafuatiliwa wanapelelezwa wanakamatwa na kisha kutiwa hatiani ,mkuu wake wa polisi na mkuu wa upelelezi walilifuatia vipi tukio hili na kuhakikisha halitatokea na wahusika imefikia hatua gani katika juhudi za kuwasaka ?

Pia ni vyema akaulizwa Waziri Mkuu na bila ya kumwacha Raisi kwani yeye ni Raisi wa Muungano kwa maana ni mhusika katika kila jambo linalohusu Muungano ULINZI ni moja wapo.
 
Kama sasa ni kazi tu ,basi kazi ifanyike hata kwa wizara Za muungano zilizopo Zanzibar hata TRA Zanzibar kuna donda ndugu !
 
Back
Top Bottom