Siku chache zilizopita nilijadiliana na ndugu mmoja kuhusu maana za maneno yafuatayo:
1) JINSI/NAMNA
Yule ndugu anadai kwamba maneno hayo yana maana tofauti:
"Bwana X hebu nieleze NAMNA/AINA ya mapokezi uliyopewa na wenyeji wako ulipotembelea Dar".
"Bwana X hebu nieleze JINSI ulivyoupenda mji wa Dar"
Licha ya hayo NAMNA siku hizi lina maana ya "a hidden agenda":
"Bw. X kuwa anakwenda kusini mwa Tanzania kila mwaka, kuna NAMNA siyo bure!!!"
"Hebu tumuulize ni NAMNA gani aliweza kupafahamu kusini mwa Tanzania?"
"Hebu nino atueleze ni JINSI gani mtu anaweza kufika kusini mwa Tanzania kwa kutumia usafiri wa Basi na ni NAMNA gani anaweza kukabiliana na misukosuko ya njiani."
2) -TIA/-WEKA
Yule ndugu anadai kwamba:
"Wazanzibari wanapendelea -TIA, lakini watanzania wengine wanapendelea -WEKA, kwa sababu neno 'kutia' lina maana ya 'kutomba' na wazanzibari wanapenda uchezeaji wa maneno"
3) DURU/MZUNGUKO
Yule ndugu anadai kwamba:
"kwenye mchezo wa mpira matumizi ya 'duru' ni sawa, lakini kwenye mchezo wa bao inafaa kutumia 'mzunguko' kwa sababu watu wengi wanachanganya 'duru ya' na 'duru za'"
Ningependa sana kusoma maoni yenu.
Asanteni.