Elections 2010 Nini Antidote ya Siasa hizi za Majitaka??????

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,667
362
……Nchi yangu Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote….
Waungwana kwa kusema ukweli hakuna kitu kinanikera kama hizi siasa za sasa hivi za majitaka. Achana na mengine mengi ila huu udini huu ndio uniafanya kutaka kufura na kupasuka kabisa. Naogopa watoto wangu kurithi upuuzi huu ambao mababu zetu hawakuturithisha ila wajinga wachache wanaasisi upuuzi huu na kuusambaza kama ushuzi.

Nimeandika kwenye makala yangu moja ndefu hapa ndani ya JF ya kuwa siasa hizi za udini kwa sasa zinatupeleka pabaya. Kibaya ni kwamba waasisi wake ndio wanaobandika wengine vibandiko hivi vya udini.

Hii imetufikisha mahali ambapo ukiongea jambo hata kama ni la msingi kiasi gani, badala ya watu kuangalia hoja yako na msingi wake, wanakutafutia kapu la dini la kukuweka humo. Hii sio tu huko vijiweni, bali hata kwa wasomi na ma-great thinkers kama wa JF waliojaliwa uwezo wa kuona kesho na keshokutwa na sio leo tu kama uono wa kuku

Kama hatutakuwa makini na kuchukua hatua historia ya siasa za udini itakuja kutuhukumu sisi na kama sio sisi basi ni vizazi vyetu vijavyo.

Hapa tulipofika kuna hatari tukafika mahali dini fulani ikawaambia wafuasi wake wazae watoto wengi zaidi kuliko wa dini nyingine ili baadae kuwa-outnumber wengine katika masanduku ya kura na mambo mengineyo mengi na mengi ambayo nawe waweza anza kuyahisi na kutaja.

Tufuatilie historia za nchi zilizokuwa na amani lakini siasa za udini zilivyozisambaratisha halafu ndipo tuone fahari za dini kukumbatia midini yetu huku tukifunga akili zetu zisijue wapi zitatupeleka. Kama dawa haipatikani mapema naamini siku moja Somalia itakuwa nchi yenye amani zaidi kuliko Tanzania yangu niipendayo.

Waungwana, wito wangu kwetu sote jamani hebu tuweke hoja zetu za udini pembeni, turudi katika hoja za msingi za utaifa. Kiongozi mbovu ni wa wote, wawe wakristo au wawe waislamu au Bahai au wahindu, ni wa wote na kama ni msoto utakuwa ni wa wote. Cement ikiwa 40,000/= Mbeya haitakula waislamu tu bali hata kwa wakristo na wahindu na hata wale wasio na dini

Niwashauri watu wote na dini zenu na msio na dini kurudi kwenye tatizo kuu la msingi la nchi yetu ambalo ni mgawanyo usio sahihi wa rasilimali za taifa unaotengeneza matabaka kati ya walionacho na wasionacho, walalahoi na walalahai n.k n.k. Tukirejea hapa msingi wa maamuzi ya taifa letu ukawa katika mambo haya ninaamini udini tutaupigilia teke mbali sana

Tuwapuuze na kuwakataa kabisa viongozi wetu wa dini wanaotaka kutuburuza kama kondoo anaeenda machinjoni kwa kutulia kimya na kufuata wakati tunajua tunaenda kuchinja. kiongozi wa dini bila kujalisaha dini yake wala wadhifa wake anaekuelekeza kuchagua mtu kwa misingi ya dini na sio mahitaji ya taifa naomba tumpige teke pembeni maana hajui anakolipeleka taifa hili. Tutumie utashi wetu kuwakataa na kufanya maamuzi kuendana na vipaumbele vyetu vya kitaifa na sio tofauti na hapo.

Waungwana, hebu ongezeni mashauri yenu hapa bila kujali itikadi ya cham au dini ya ni namna gani tunaweza kuitoa nchi yetu katika siasa chafu za udini ambazo zitakuja kuumiza vizazi vyetu wakati hawa wanaopanda mbegu hii watakapokuwa hawapo au wamewahamishia watoto wao Ulaya na kwingineko

Nawasilisha hoja kwenu waungwana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom