Ningekuwa rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningekuwa rais

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JamboJema, Mar 9, 2012.

 1. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Madktari wapo kwenye mgomo usionakikomo. Mengi yanasemwa kuhusiana na mgomo huu. Wapo wanaodai madaktari wamekosea KUMWAMRISHA rais kwamba awatimue kazi waziri wa afya na naibu wake. Wapo wanaoona madaktari wapo sawa kwani madai yao yalikuwa ni moja ya makubaliano waliyowekeana na waziri mkuu.

  Wanaowapinga madaktari wanahoja moja nzito kuwa iwapo rais atakubaliana nao na hivyo kuwatosa akina Mponda, basi huo ndio utakuwa utaratibu mpya Tanzania ambapo sasa pengine walimu wanaweza pia kuja na dai la kumkataa waziri! Kwao hii ni hatari kubwa na jambo lisilokubalika. Kwao Rais ni taasisi isiyotakiwa kuelekezwa na yeyote aliye chini. Ni yenyewe tu ndo inauwezo wa kuelekeza na si kuelekezwa!

  Nawaunga mkono madaktari kwani imekuwa ni utamaduni wa taasisi ya urais kutokutaka kusikiliza katika majadiliano. Angalia suala la akina Hosea, Mnyika n.k. Pengine huu utaratibu wa sasa wa madaktari ni mwarobaini wa tatizo hili.

  Naomba niwe muwazi kuwa kwa hili siwaungi mkono wanaowapinga madaktari. Rais tunamchagua sisi ili atutumikie. Hatumchagui atutumie. Tunahitaji atutumikie na hivyo ni wajibu wetu kumweleza pale anapotenda ndivyo sivyo ili aparekebishe. Leo rais anaongea na wazee wa Dar es salaam. Naamini anafanya hivi kujaribu kuwapinga madaktari.

  Ningekuwa mimi ni rais, ningeutumia mkutano huu kuwaondoa akina Mponda na kutoa onyo kali kwa mawaziri wengine WANAOSHINDWA KAZI kuwa hili litawakumba pia. Haitakiwi kulea wateule wako hadi watu wafikie mahala pa kutaka wewe sasa uondoke kwa sababu wateule wako wameshindwa kazi! Hii ingewafanya mawaziri na wateule wengine wa rais kuanza kuwajibika kwa wananchi na si kwa rais pekee.

  Haya nayasema kwamba iwapo tu ningekuwa rais...! Naomba rais wangu alione hili katika kona hii ili tusiendelee kufa kwa sababu ya watu wawili tu anaowapenda sana kuliko maisha yetu.

  JUST THINKING ALOUD!
   
 2. R

  REAL PASTOR Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inahitajika hekima ya MUNGU sana kwa swala hili.Pande zote kunaonyesha hatari fulani!LAKINI LAZIMA MOJA LIFANYIKE!!Sijui ningekuwa Raisi ningemwendea nani anipe HEKIMA KAMA YA MFALME SULEMANI!!!
   
Loading...