Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 279
- 389
1. Kwakuwa Rais ni Mwenyekiti wa CCM, linapotokea jambo linalohusu ufafanuzi, Msemaji wa Chama awe mmoja tu, mengine yawe ni maoni tu ya Wanachama na upande wa Serikali vivyo hivyo msemaji ni mmoja tu. Sio kwamba wasemaji hawapo lakini shida ni kwamba wanaruhusu kauli zisizo rasmi kuonekana kuwa ni msimamo wa Chama na ni msimamo wa Serikali. Communication Professionalism inakosekana.
🔸Hii itasaidia Chama Pamoja na Serikali kutokujichanganya Katika kauli zake zinazoleta utata kutoka Kwa makundi mbalimbali na wapambe binafsi ambapo Kila wakijiskia kutoa majibu muda wowote wanaitisha Press na kuanza mashambulizi kwa Hisia na sio kutoa majibu kulingana na Hoja.
🔸Tumeshuhudia kauli nyingi mseto kuanzia chipukizi, uvccm, jumuiya mbalimbali mpaka Wanachama binafsi na wapambe wa Serikali wakiwajibu wanaoibua hoja kwa kuhitaji majibu. Lakini wanajibiwa kwa kushambuliwa, kejeli na mipasho bila viongozi wa Chama na Serikali kukemea na kukanusha kuwa haya sio majibu ya Chama wala Serikali, hii inachochewa na tabia ya uchawa. Kila mtu anapojiskia anaitisha Press hii idhibitiwe.
Likiwezekana hili,Chama na Serikali vitapiga hatua kuimarisha uhusiano mzuri na Wananchi.
2. Ningemshauri Rais kuwa ashirikiane na mawakili wa Jamhuri awashauri kuachana na Kesi ya Tundu Lissu, na mshitakiwa aachiliwe Huru.
🔸 Kwanini? Kwasababu kuendelea kumshikilia kunampa umaarufu zaidi Kisiasa katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa. Anajengewa Public attention kubwa ni Bora hata asingeshitakiwa.
🔸 Sababu nyingine kwanini Lissu aachiwe ni kwaajili ya kuimarisha "Umoja wa Kitaifa" na kuondoa Chuki.
3. Suala la Watu kutekwa, kupotezwa, Ningemshauri Rais kwamba liundiwe TUME mseto na Huru kuchunguza na kuwabaini wahusika ili wachukuliwe hatua kali kwa kuichafua Serikali na "icon" ya Urais. Hii itasaidia kurudisha imani Kwa Wananchi na kuondoa hofu ya watu kutekwa.
4. Ningemshauri Rais kuwa Mchakato wa Uchaguzi ufanyiwe Maridhiano kwa kushirikisha wadau wote, wazee wastaafu, viongozi wa Dini na asasi za kiraia ili vyama vyote vishiriki Uchaguzi. Makubaliano yafanyike kipi kiondolewe kipi kiwepo.
🔸Hakuna sababu ya CCM kuogopa marekebisho na madai ya Upinzania. CCM ina mambo mengi ya kujinadi Kwa Wananchi kuliko Upinzania hakuna haja ya kuogopa. Tofauti na hapo labda kama kuna watu wenye kuinadi Ilani ya Chama na utekelezwaji wake kwa mihemko ya uchawa.
TAIFA MOJA, SAUTI MOJA.

Tukumbuke wapo wanaccm na watu wa serikalini ambao hawafurahishwi na Lissu kushikiliwa, sio kwasababu wanampenda sana ila kwasababu anasababisha Mataifa ya Nje kutumulika na kutuangalia Kwa jicho la karibu zaidi, kitu ambacho sio kizuri Kwa ustawi wa Taifa.
3. Suala la Watu kutekwa, kupotezwa, Ningemshauri Rais kwamba liundiwe TUME mseto na Huru kuchunguza na kuwabaini wahusika ili wachukuliwe hatua kali kwa kuichafua Serikali na "icon" ya Urais. Hii itasaidia kurudisha imani Kwa Wananchi na kuondoa hofu ya watu kutekwa.
4. Ningemshauri Rais kuwa Mchakato wa Uchaguzi ufanyiwe Maridhiano kwa kushirikisha wadau wote, wazee wastaafu, viongozi wa Dini na asasi za kiraia ili vyama vyote vishiriki Uchaguzi. Makubaliano yafanyike kipi kiondolewe kipi kiwepo.
🔸Hakuna sababu ya CCM kuogopa marekebisho na madai ya Upinzania. CCM ina mambo mengi ya kujinadi Kwa Wananchi kuliko Upinzania hakuna haja ya kuogopa. Tofauti na hapo labda kama kuna watu wenye kuinadi Ilani ya Chama na utekelezwaji wake kwa mihemko ya uchawa.
TAIFA MOJA, SAUTI MOJA.
>Aluta Continua<<<