Ninakubaliana nanyi mkuu
Kigarama na mkuu
Mpenda Yesu,
Hapa nadhani kuna mambo kadhaa yanayochangia,
1. Jamii.
Jamii/asilimia kubwa ya wakazi bado hawana elimu ya kutosha ya uraia, na kama wanayo bado hawajaelimika/kuitumia vyema/ipasavyo.
Hii husababisha kufanya mambo kwa mazoea, kujuana, kimzaha.Hata inapokuja kwenye kuchagua viongozi mengi hutokea, kuchagua viongozi kutokana na mmoja wa wanafamilia/ukoo alikuwa kiongozi(mf. baba, mama, shangazi, mjomba n.k).
Pili wanajamii kuhofia mabadiliko na hivyo kufanya mambo kwa mazoea.
2. Viongozi:
Viongozi wengi wanasiasa/na wale wasio wanasiasa kupuuzia mambo, mf. Kiongozi kwa kutambua wazi maslahi ya Taifa hili ni haya na yeye kufanya kinyume.
Nakosa maana ya maneno haya "to take advantage" ya ujinga(kutokufahamu) kwa wananchi.Hata pale penye kuhitaji hekima ndogo bado ulaghai utahusishwa.
3. Mfumo:
Kila chama kinasema kikishika hatamu kitafanya haya na haya, na chama tawala kama ambavyo 'kimeshafanya' ya kwake.
Iwapo tutakuwa na mfumo fulani(mf. kama wa nchi ya Marekani) yaani, ingawa kuna vipaumbele vya kila chama, lakini chama chochote kitashika uongozi vipaumbele vya Taifa vitaanza kutekelezwa yaani vile vya muda mfupi(short term) na vile vingine vya Chama husika vitafuata vikienda sambamba na vile vya muda mrefu(long term goals) katika kutekelezwa.
Pili, kuna kitu fulani huwa nikijiuliza..katika makampuni binafsi, mashirika tunapitisha Usaili(Interview) tukichambua sifa mbali mbali za watu, hasa tukiangalia viwango vya elimu na uzoefu. Lakini inapokuja kwenye viongozi wa Taifa(ngazi mbali mbali) vigezo vitakuwa ni
1. Awe Raia wa Tanzania
2. Awe na umri kadhaa
3. Asiwe na kosa/makosa ya jinai
4. AWE ANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA.
5. N.k
Sasa unajiuliza iwapo viongozi tunaowachagua hatutilii mkazo sana katika Elimu, tunategemea tupate viongozi gani? Kwa mfano hebu tazama Elimu ya watendaji wa mhimili mmoja(Bunge)!Ni aibu karibu au zaidi ya asilimia hamsini(50%) wawe na elimu ya msingi.
Ufikiri, Upana, Utatuzi wa mambo utakuwa mdogo tu.
Tatu, adhabu mbalimbali hasa kwa viongozi(hasa wanasiasa) wenye kurudisha maendeleo hupuuzwa, mf. kiongozi anapojiuzulu, anapoomba radhi ili hali ameleta hasara kwa Taifa, wananchi(Jamii) huridhika bila kujali kilicgopungua, hata katika chama husika viongozi kama hawa huendelea kushika hatamu mbali mbali!
Sasa wanasiasa wachanga(makinda/chipukizi) huiga mifano hii hii na kuiendeleza.
Hivyo, Jambo na 3 hapo juu hutegemea sana jambo namba 2 ambalo hutegemea jambo namba 1. Mambo haya matatu(niliyoyataja hapo juu) huchangia sana katika kubadilisha(kwa kusonga mbele) siasa ya nchi.