Ninatafuta kazi ya kufundisha

Ninatafuta kazi ya kufundisha

Natafuta pesa

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
287
Reaction score
396
Habari,

Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 24 ni muhitimu wa elimu ya juu, nina shahada ya elimu niliyoipata mwaka jana (2022),

Nina uzoefu wa ufundishaji usiopungua mwaka mmoja, kwa sasa nipo Dar es Salaam maeneo ya Gongo la mboto,

Nina uhitaji wa nafasi ya kazi ya kufundisha iwe kwa "part time" au "full time",

Kwenye shule za sekondari, vyuo vya kati vya elimu, "Tuition centers", primary school (standard one-seven/six), majumbani,

Hata kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohitaji wawezeshaji, pia nipo tayari,

Lakini inawezekana kote huko kunakohusiana na taaluma yangu hii kusiwe na nafasi,

Kama pia kutakuwa na hata kibarua cha kwenda na kurudi hata chenye uhakika wa posho ya angalau 20k per day basi pia nipo tayari,

Tuwasiliane kupitia PM, kwa madodoso zaidi kwa mdau atakayekuwa na hiyo nafasi iwe ni direct au indirect,

Ninawasilisha.
 
Asante sana kwa ushauri, nimeupokea inshallah nitaufanyia kazi.
Kuna muda utahitajika kuweka vyeti pembeni na kupambana na uhalisia; maisha lazima tuyaishi, uwe na ajira au usiwe na ajira; swali, Je utakula nini?
 
Kuna muda utahitajika kuweka vyeti pembeni na kupambana na uhalisia; maisha lazima tuyaishi, uwe na ajira au usiwe na ajira; swali, Je utakula nini?
Ni kweli hasa hapo kwenye kupata mahitaji ya msingi, najaribu kote kote ngoja nione.
 
Back
Top Bottom