Ninapoangalia utawala wa Kikwete na kulinganisha na Dr. Magufuli

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Nikikaa na kuangalia utawala wa Kikwete na kuulinganisha na wa Magufuli. Naona wa Magufuli una nafuu mara 1000. Sasa angalau kuna nidhamu ya kiwango kikubwa sehemu mbalimbali.

Miaka ile ya nyuma mambo yalikuwa hovyo ulikuwa ulimwengu wa kambale. Baba sharubu na watoto sharubu. Sasa nidhamu ipo kwa kiwango kikubwa sana kuanzia kwenye chama hadi nje ya chama.

Ule wizi wa mabilioni hatujausikia kwa muda mrefu angalau tunapata faraja hakuna familia inayotuibia na kujitajirisha yenyewe tu.

Mh Magufuli ana udhaifu wake lakini udhaifu wake una nguvu zaidi ya nguvu za mtangulizi wake.
 
Utawala uliopita ulikuwa mzuri sana katika kufuata taratibu za kisheria mpaka wakati mwingine ulikuwa unakera..nakumbuka suala la majaji wa escrow,rais Kikwete alikuwa analaumiwa kwa kutokukurupuka kuwafukuza wale majaji!

Mapungufu ya utawala huu ni kile kinachoonekana kama kujaribu kuzipuuzia taratibu za kisheria, uwepo wa kila mtu kutaka kutoa matamko na kuonekana mwenye mamlaka na uwepo wa kauli tata zisizobeba faraja kwa wananchi wake!

Mbali na hayo nidhamu imeongezeka kwa kiasi kikubwa!
 
Tatizo la huyu wa sasa, uongozi wake ni wa hovyo. Hazingatii protokali wala katiba. Hatafanikiwa.
 
Kuwa Kiongozi Mzuri Ni Kuwa Mkali Bila Kufuata Sheria?Au Ni Yule Anayefuata Katiba Na Kanuni Za Sheria
 
Nikikaa na kuangalia utawala wa Kikwete na kuulinganisha na wa Magufuli. Naona wa Magufuli una nafuu mara 1000. Sasa angalau kuna nidhamu ya kiwango kikubwa sehemu mbalimbali.

Miaka ile ya nyuma mambo yalikuwa hovyo ulikuwa ulimwengu wa kambale. Baba sharubu na watoto sharubu. Sasa nidhamu ipo kwa kiwango kikubwa sana kuanzia kwenye chama hadi nje ya chama.

Ule wizi wa mabilioni hatujausikia kwa muda mrefu angalau tunapata faraja hakuna familia inayotuibia na kujitajirisha yenyewe tu.

Mh Magufuli ana udhaifu wake lakini udhaifu wake una nguvu zaidi ya nguvu za mtangulizi wake.

Siyo sahihi kuzilinganisha tawala hizi mbili kwa sababu: JK ametawala kwa miaka 10 na JPM ndo ana mwaka mmoja tu. Kumbuka hayo ma-Esrow na madudu mengine hayakujulikana ndani ya mwaka mmoja. Kupata ulinganifu sahihi tumpe mda JPM angalau miaka 5
 
Mleta maada hujui kulinganisha, unawezaje kulinganisha mtoto wa mwaka mmoja na mtoto wa miaka kumi. Au umetumia minajihi gani,?????? Vuta muda "THE TRUE JUDGE IS TIME"
 
Back
Top Bottom