Ninaomba ushauri wa kuachana na vimeo

gepema

Member
Mar 25, 2010
97
9
Wanajavamvi mimi ni mgeni huku nipo sana jukwaa la siasa leo naomba ushauri wenu wanajamvi la mapenzi.
Jamani nina tatizo ambalo natamani kuachana nalo lakini bado sijaweza.

Nina mke mzuri, watoto wazuri na maisha mazuri sema mimi ni malaya "MBWA" sio neno zuri kulitumia lakini huo ndio ukweli. Nimeshakuwa na mahusiano na zaidi ya wanawake tisini(90) na hivi sasa kuna wanawake kumi(10) ambao kila mmoja anajihesabu kwamba yupo yeye na mwenye mali tu(wife).

Dhamira inanisuta sana wakati nikimtazama mke wangu na upendo wake kwangu wakati mimi namgawia utamu wake nje, namshukuru Mungu sina ukimwi wala sijawahi kupata ugonjwa wowote wa zinaa.

Mwanzo nilikuwa malaya sana mpaka niliposema nataka kuoa home wakaniuliza kama ni kweli nipo serious au nataka kuwatia aibu nikawaambia nipo serious mchakato ukaendelea nikaoa, baada ya hapo nilikaa kwa miaka mitano bila kuwa na mahusiano nje ghala akatokea shemeji yangu akanitamkia mwenyewe baadae nikamchukua na ndio ukawa mwanzo mpya, nikaendeleza tabia yangu mpaka sasa!

Kila demu ninayemtokea huwa hanikatalii hii imenifanya niwe kiwembe mpaka leo!
Mke wangu nampenda sana na yeye ananiamini lakini mumewe ni malaya sana.

Je nifanyeje ili kuacha hii tabia coz najua kwamba mwisho wa siku wale wadada ninaowaacha huwa wanaumia maana unakuta wamekolea wakati mimi tayari naendelea kwa mwingine.

NAOMBA MSAADA WENU JAMANI
 
Msaada gani mwingine unataka zaidi ya wewe mwenyewe kuamua kwamba hutaki tena kua hivyo?!

Amua na utekeleze...hicho ndicho unachohitaji kufanya!
 
Gepema kwanza nikupongeze kwa hatua hii ya ujasiri ya kusema udhaifu wako...ni mwanzo mzuri kwa kua ni step moja katika kuelekea njia ya ushindi...Ni jambo zuri na la kujivunia sana kuwa na wanawake wengi so far una utilize uana ume wako lakini kuna swali dogo sana la kujiuliza,mwisho wa yote nini hatima yake! Umekiri mwenyewe kwamba una mke mzuri na aliyekuzalia watoto wazuri as well,kwanini usimsaidie mkeo kuendeleza familia na badala yake umwingize tena kwenye risk ya magonjwa kutokana na matendo yasiyofaa?

Mimi nadhani hujafika mbali kiasi cha kushindwa kuacha,hebu kua mtumwa wa maamuzi magumu ya kuwa mtu safi na baada ya miaka mitano utaniambia hata kimaendeleo utakua wapi!
 
Mkuu utakua una hela sana,ndio maana mademu wanaku mind,mademu wanapenda watu waliooa wanakufanya kama Atm,cha kufanya anzisha project inayohitaj alot of money,then watakukimbia mmoja mmoja.
 
Kwenye maombi sijawahi kwenda sema kila ninapoenda kanisani huwa lazima nimuombe Mungu anisaidie kuacha hii tabia
 
Sas na wewe tisini umeona wengi kuna mwanaume mmoja aliwahi kunambia wanawake aliolala nao wanajaa dar express kumi. BTW: Fanya kitu kitakachokuweka busy
 
Tengeneza mazingira ya kuwa karibu sana na familia/mkeo kila wakati bila kusahau kusali.
 
Duhhhhhhh
Kwanza napenda kukupa hongera
Kwa vitu vitatu...
1. Kugundua na kukubali kosa
2.kuelewa umuhimu wa mkeo kwako
3.kukiri waelewA ni jinsi gani unawaumiza
Hao wanawake wengine uwaachapo...

Well
Kwa maelezo yako "you're addicted " huna
Tofauti na mtu ambae ni alcoholic or smoker
Sasa umeshatuhakikishia kwamba waweza
Kuacha ukitaka.. " uliacha kwa muda wa miaka mutano " ushauri wangu rudi nyuma
Chunguza nini kilikufanya uache kwa muda huo muda " miaka mitano"
Kama ni watoto, mke au familia kwa ujumla
Basi punguza muda kwenda out na
Concentrate kwenye hicho kimojawapo au
Vyote...

Kama hilo litakuwa ngumu ku archive
Mwenyewe basi tafuta professional help
" cancelling " ....
 
Sasa huko kote ulikopita si nyama ni ile ile, sasa kinachokufanya usiachane nao ni nini. usijigambe kuwa huna ukimwi kaka hapo ulipo teyari ni muathirika tena mpeleke na mkeo akapime. mimi niko kwenye study ya ukimwi naomba contact zako maana tunatafuta watu kama nyie ambao mnamsambaza ukimwi ila vile vijidudu haviwazuru zamani kwa makosa mlikuwa mnaitwa (Caria).
 
DuhhhhhhhKwanza napenda kukupa hongeraKwa vitu vitatu...1. Kugundua na kukubali kosa2.kuelewa umuhimu wa mkeo kwako3.kukiri waelewA ni jinsi gani unawaumiza Hao wanawake wengine uwaachapo...WellKwa maelezo yako "you're addicted " hunaTofauti na mtu ambae ni alcoholic or smokerSasa umeshatuhakikishia kwamba waweza Kuacha ukitaka.. " uliacha kwa muda wa miaka mutano " ushauri wangu rudi nyuma Chunguza nini kilikufanya uache kwa muda huo muda " miaka mitano"Kama ni watoto, mke au familia kwa ujumlaBasi punguza muda kwenda out na Concentrate kwenye hicho kimojawapo auVyote...Kama hilo litakuwa ngumu ku archive Mwenyewe basi tafuta professional help" cancelling " ....
Kibuyu kinafanya kazi ehhhhh?!
 
Wanajavamvi mimi ni mgeni huku nipo sana jukwaa la siasa leo naomba ushauri wenu wanajamvi la mapenzi.
Jamani nina tatizo ambalo natamani kuachana nalo lakini bado sijaweza. Nina mke mzuri,watoto wazuri na maisha mazuri sema mimi ni malaya "MBWA" sio neno zuri kulitumia lakini huo ndio ukweli. Nimeshakuwa na mahusiano na zaidi ya wanawake tisini(90) na hivi sasa kuna wanawake kumi(10) ambao kila mmoja anajihesabu kwamba yupo yeye na mwenye mali tu(wife).
Dhamira inanisuta sana wakati nikimtazama mke wangu na upendo wake kwangu wakati mimi namgawia utamu wake nje,namshukuru Mungu sina ukimwi wala sijawahi kupata ugonjwa wowote wa zinaa. Mwanzo nilikuwa malaya sana mpaka niliposema nataka kuoa home wakaniuliza kama ni kweli nipo serious au nataka kuwatia aibu nikawaambia nipo serious mchakato ukaendelea nikaoa,baada ya hapo nilikaa kwa miaka mitano bila kuwa na mahusiano nje ghala akatokea shemeji yangu akanitamkia mwenyewe baadae nikamchukua na ndio ukawa mwanzo mpya,nikaendeleza tabia yangu mpaka sasa! Kila demu ninayemtokea huwa hanikatalii hii imenifanya niwe kiwembe mpaka leo!
Mke wangu nampenda sana na yeye ananiamini lakini mumewe ni malaya sana,je nifanyeje ili kuacha hii tabia coz najua kwamba mwisho wa siku wale wadada ninaowaacha huwa wanaumia maana unakuta wamekolea wakati mimi tayari naendelea kwa mwingine!!!
NAOMBA MSAADA WENU JAMANI

Jukwaa la siasa watakushauri vizuri sanasana Mzee Ngeleja:))lol

Ukiwa na nia&dhamira lazima utakamilisha jambo!..Tubu, kapime ukimwi tena, acha mawasiliano na hao wanawake 90 halafu tulia na mkeo muijenge familia yenu..Mpe mambo mkeo wakati una nguvu sio unazimalizia nje halafu ukishazeeka ndiyo utulie na kumzeekea zaidi.
 
Tatizo lako kaka laweza kuwa la kisaikolojia zaidi (kama ugonjwa) kawaone watu wa ushauri nasaha wakusaidie kubadili tabia kwani naona huko addicted
 
Bwana Gepema kwanza nianze kwa kukupongeza kwa kuuweka uwazi wako kwenye jamvi hili, pili naona sasa ndiyo umeanza kuzinduka na kugundua kwamba kuwa na wanawake wengi hakuna tija kwa afya yako na familia yako. Tatu ni mapendekezo yangu

1. Kitu cha kwanza wewe ni muongo sana! kwanini? unamdanganya mke wako unampenda kumbe uwongo, unawadanganya wanawake huna mke/au yeye ndiye unatarajia kumuoa, inawezekana na sisi hapa pia umetudanganya! cha kufanya jaribu kuwa mkweli na uache uwongo! Nina uhakika haovimada wako ukiwaambia ukweli unampenda mke wako kuliko wao kama ulivyosema watakimbiwa wenyewe.

2. Punguza tamaa, ngono ipo na itaendelea kuwepo, wanawake wazuri wapo na wataendelea kuwepo huwezi kuwamaliza hata kama ukilala na mwanamke mmoja mmoja kila siku hadi mwisho wa maisha yako. Ushapanga kuoa maana yake ulipanga na kumchagua mkeo huyo mzuri kuliko wote. hao wengine waharibufu achana nao au hukuridhika na mkeo? kaa tulia na ujiulize nini umekosa kwa mkeo hadi uwafate hao unaowaita vimeo. Utagundua hakuna jipya kaka, leo watoto wako watakufaa muda wote uzeeni kuliko kuhangaika na vimeo wanaokufaa kwa dakika tu wakati ukiwa nacho

3. Jipe mazoea ya kutoka na mke wako wakati wa weekend, vimeo wachache wakimwona wanaweza kukukimbia
4. Acha kuhonga mkuu, somesha watoto. kama unasema hakuna vimeo wanaokukataa ukitia neno inaonekana wewe unachukua wanaojiuza na unamwaga pesa nyingi! ndo mana hawakatai weweeee! Ukutane na wanawake wenye msimamo bwana wala usingewaita vimeo! unapigwa chini na vijisenti vyako!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom