Ninahitaji kazi

Ninahitaji kazi

Joined
Feb 15, 2021
Posts
77
Reaction score
89
Poleni na majukumu ndugu zangu. Mimi ni kijana was kiume, nina umri wa miaka 27 na ninaishi Dar es salaam Tanzania.
Ninahitaji kazi, aidha internship, nafasi ya kuanzia(entry level), kazi ya kujitolea inayolipwa au nafasi za junior. Nina shahada ya Sayansi ya Maji na Uvuvi (Bsc.Aquatic Science and Fisheries).

Katika safari yangu kwa vipindi tofauti nimetekeleza baadhi ya majukumu ikiwa ni pamoja na wakala wa mauzo wa moja kwa moja, msimamizi wa mauzo ya Hoteli, wakala wa Usambazaji, Mtu wa Masoko, Mkusanya Mapato, Afisa wa Uvuvi wa Kujitolea, Mhifadhi wa Mazingira na mwalimu rika.

Majukumu yoyote kati ya yaliyotajwa ninaweza kutoshea. Pia nimefanya mafunzo kuhusu utoaji wa mkopo na ukusanyaji wa awamu nikimaanisha kuwa naweza pia kufanya kazi kama afisa wa mikopo.

Nina ujuzi wa kutumia kompyuta, mawasiliano (communication and customer service skills), ushawishi na usuluhishi wa matatizo pamoja na ujuzi mwingine unaofanana na huo. In mchapakazi na kwenye malengo. Pia njna uwezo mkubwa was kujifunza kwa haraka na nina shauku ya kuyafikia matokeo.

Tafadhali nahitaji maoni yako na msaada wako na ikihitajika naweza kutuma CV yangu kwa ukaguzi wako.

Asante.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb

Similar Discussions

Back
Top Bottom