Ninachowaza juu ya Rais Magufuli

Ninachowaza juu ya Rais Magufuli

SBAKARI

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2016
Posts
355
Reaction score
289
Nikiri tu kwamba nami ni mmoja wa watu ambao naiona dhamira ya dhati ya Mh. Rais wa awamu ya tano katika kulisaidia taifa letu. Kutokana na kauli zake na matendo yake ni wazi Mh. ana kiu ya kuona mabadiliko ya haraka kwa nchi yetu. Mh. anatamani kuona kila mtu anatembea kwenye nyayo zake ili kuifikia kwa haraka dhamira yake njema. (Ingawa kuwa na dhamira njema pia kunategemea sana njia bora za kuifikia dhamira hiyo)

Kitu nachokiona, kuanzia mh. mwenyewe mpaka wafuasi wake yaani sisi tunaoamini katika dhamira yake njema, tunaona kabisa kwa muda wa kikatiba uliopo ni ngumu kuifikia dhamira njema aliyo nayo mh. Na hapo ndipo tatizo linapoanzia. (

Kutokana na athari za kuona muda ni mdogo, mh. amekuwa akitaka mambo mengi yabadilike kwa haraka kitu ambacho ni ngumu kutokea, matokeo yake ndipo watu wanaona kama mh. anakurupuka kumbe la hasha ni kule kutaka kukimbizana na muda tu.

Kwa upande wa wafuasi nao wameshindwa kabisa kuamini kwamba baada ya muda huu mfupi kuisha atatokea mtu mwingine atakayekuwa na dhamira ya dhati kama ya Mh. JPM. Wengi nikiwepo na mimi tuna wasi wasi pengine mtu ajaye anaweza akaturudisha kule kule tulipotoka, ndipo sasa wanapoona suluisho pekee ni kumuongea muda Mh. JPM (Hapo ndipo tunapoachana na wenzangu walio wengi)

Angalau juzi nimemsikia Mh. Kule Kigoma akitamka kwamba yeye anataka amtengenezee Rais anayemfuata njia ya kuongoza vizuri. Tena akajifananisha na Yohana wa katika Biblia aliyemtayarishia mapito Yesu/Issa bin Mariam. Kumbe Mheshimiwa ana mpango hata wa kutaka kuongezewa muda. Kwa maelezo hayo ina maana wale wanaotaka mh. aongezewe muda wana hoja lakini kuna sehemu moja tu ambayo hawafiki; Tumeshuhudia huko nyuma wakuu wa nchi wakibadilisha badilisha mambo mengi kulingana na wanavyoona inafaa. Mengine yalileta manufaa, na mengine ndio yametufikisha kwenye matatizo haya tuliyo nayo leo.

Sehemu pekee ambayo wenzangu hawataki kufika ni kwenye marekebisho ya katiba. Baba yetu Magufuli chonde chonde tuachie katiba mpya baba. Na katiba hiyo si nyingine ni ile ya Mh. Warioba. Kwa kutupa/kutuachia katiba safi, si tu itakupa heshima na kudhihirisha wazi dhamira yako njema, bali itafanya hata anayekufuatia kutokuturudisha kule kule
 
Miaka yote 5 aache katiba tu? umeongea utumbo mkuu, tunataka maendeleo kama nyie CCM hamuwezi achieni wengine.
 
Naunga mkono hoja. Uwe unapita pita na mtaa huu Shunie japo saa moja tu kwa siku. Usisahau pia kuwaita na wale marafiki zako pia 😛😛😛

Mstari wa mwisho ndio nimekuelewa mkuu sanaa yaan huko kwa mwanzo jisemee mwenyewe
 
Naunga mkono hoja. Uwe unapita pita na mtaa huu Shunie japo saa moja tu kwa siku. Usisahau pia kuwaita na wale marafiki zako pia 😛😛😛
Sawa kaka BAK jamaan nitakua napita nitaiwata na wenzangu
 
Nikiri tu kwamba nami ni mmoja wa watu ambao naiona dhamira ya dhati ya Mh. Rais wa awamu ya tano katika kulisaidia taifa letu. Kutokana na kauli zake na matendo yake ni wazi Mh. ana kiu ya kuona mabadiliko ya haraka kwa nchi yetu. Mh. anatamani kuona kila mtu anatembea kwenye nyayo zake ili kuifikia kwa haraka dhamira yake njema. (Ingawa kuwa na dhamira njema pia kunategemea sana njia bora za kuifikia dhamira hiyo)

Kitu nachokiona, kuanzia mh. mwenyewe mpaka wafuasi wake yaani sisi tunaoamini katika dhamira yake njema, tunaona kabisa kwa muda wa kikatiba uliopo ni ngumu kuifikia dhamira njema aliyo nayo mh. Na hapo ndipo tatizo linapoanzia. (

Kutokana na athari za kuona muda ni mdogo, mh. amekuwa akitaka mambo mengi yabadilike kwa haraka kitu ambacho ni ngumu kutokea, matokeo yake ndipo watu wanaona kama mh. anakurupuka kumbe la hasha ni kule kutaka kukimbizana na muda tu.

Kwa upande wa wafuasi nao wameshindwa kabisa kuamini kwamba baada ya muda huu mfupi kuisha atatokea mtu mwingine atakayekuwa na dhamira ya dhati kama ya Mh. JPM. Wengi nikiwepo na mimi tuna wasi wasi pengine mtu ajaye anaweza akaturudisha kule kule tulipotoka, ndipo sasa wanapoona suluisho pekee ni kumuongea muda Mh. JPM (Hapo ndipo tunapoachana na wenzangu walio wengi)

Angalau juzi nimemsikia Mh. Kule Kigoma akitamka kwamba yeye anataka amtengenezee Rais anayemfuata njia ya kuongoza vizuri. Tena akajifananisha na Yohana wa katika Biblia aliyemtayarishia mapito Yesu/Issa bin Mariam. Kumbe Mheshimiwa ana mpango hata wa kutaka kuongezewa muda. Kwa maelezo hayo ina maana wale wanaotaka mh. aongezewe muda wana hoja lakini kuna sehemu moja tu ambayo hawafiki; Tumeshuhudia huko nyuma wakuu wa nchi wakibadilisha badilisha mambo mengi kulingana na wanavyoona inafaa. Mengine yalileta manufaa, na mengine ndio yametufikisha kwenye matatizo haya tuliyo nayo leo.

Sehemu pekee ambayo wenzangu hawataki kufika ni kwenye marekebisho ya katiba. Baba yetu Magufuli chonde chonde tuachie katiba mpya baba. Na katiba hiyo si nyingine ni ile ya Mh. Warioba. Kwa kutupa/kutuachia katiba safi, si tu itakupa heshima na kudhihirisha wazi dhamira yako njema, bali itafanya hata anayekufuatia kutokuturudisha kule kule
Uzi wako unaonyesha una "k" poa sana.
 
Back
Top Bottom