Ninachokiona kwenye mechi kati ya Ufaransa na Ureno

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,135
48,821
1: UFARANSA.

Ukiachana na aina ya wachezaji walio nao, ile hali ya kuwa mwenyeji kwenye michuano hii itamfanya aanze kwa kushambulia ili apate goli la mapema. Kitu hiki alikikosa kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani kwa sababu Ujerumani walikuwa na Toni Kroos na Ozil ambao walikuwa wanauwezo mkubwa wa kupiga pasi hivo kuifanya Ujerumani kuwa na Mpira . Endapo itatokea kwenye mechi hii ya Fainali kwa Ufaransa kushindwa kupata goli mwanzoni itawaumiza sana kadri muda wa mchezo utakavyokuwa unazidi kwenda.

UPI UBORA WA UFARANSA?.

Sehemu kubwa inayoijenga na kuipa nguvu Ufaransa kuelekea mechi hii ni mashabiki. Kucheza nyumbani kutawapa nguvu na sababu ya kushinda na kubakisha kombe hili.

Pili, kwenye Mashambulizi Ufaransa wamekuwa wakitengeneza msukumo mkubwa wa mashambulizi kwa kuanzia eneo la kiungo . Uwepo wa Pogba, Matuidi, Payet umekuwa msaada mkubwa kwenye utengenezaji wa mashambulizi na hapa ndipo ubora wa Ufaransa unaanzia . Wamekuwa ni viungo wenye hasira, wabunifu katika kutengeneza nafasi za kufunga magoli . Na hii moja kwa moja inaifanya safu ya ushambuliaji ya Ufaransa kuwa hatari ikiwa na Antoine Griezmann.

UDHAIFU WA UFARANSA……………

Udhaifu wa ufaransa upo kwenye safu ya Ulinzi. Ubora wa ukabaji wa Evra umepungua kwa kiwango kikubwa sana, hii imekuwa ikiigharimu timu pindi inapokuwa inashambuliwa kwa kasi kupitia upande wa kushoto, ukizungumzia ubora wa Evra kupungua utakuwa hujatenda haki kumzibia mdomo Sagna. Kwa hiyo hali hii hufanya mabeki wa kati kupata kazi ya kuzuia sana mashambulizi yanayokuja kwao. Na ukiangalia vizuri Koscienly hajapata pacha sahihi wa kucheza naye pale kati ya Umtiti na Rami ambao wamekuwa wanamakosa mengi binafsi.

KIPI WAKIFANYE UFARANSA ILI WASHINDE ?

Ukiwaangalia Ureno kwenye michuano hii, imekuwa timu inayocheza mchezo usiovutia , imekuwa ikikaba sana kwa nidhamu ya hali ya juu, na kuwasubiri wapinzani wao wafanye makosa na kuwaadhibu, hivyo kupata ushindi kwa aina ya timu ya Ureno unatakiwa kwanza kabisaa uwe na kiungo mwenye nusu ya tabia ya aina ya uchezaji wao, yani kiungo anayeziba njia ya mipira, anayeharibu mipango ya timu pinzani na kutengeneza kwa haraka mipango ya timu yake. Kwa mantiki hiyo naonelea Ng’olo Kante atakuwa mtu sahihi kuanza kwenye mechi hii. Na kama Kante akianza , Ufaransa hawatakiwi wacheze mfumo wa 4-3-3.Wakicheza mfumo huu ingawa utamfaa moja kwa moja Kante,lakini mbele kutakuwa kumepungua kitu kimoja kikubwa nacho ni Griezmann kucheza kulia ,hali ambayo haitakiwi kwani ubora wa safu ya ushambuliaji ya Ufaransa huwa pale Griezmann anapotokea nyuma au karibu na Giroud. Hivyo Kitu ambacho kitatatiwa ni Kucheza kamari ya kutomwanzisha Matuidi . Na akiacha kumwanzisha Matuidi watalazimika kucheza 4-1-3-2……

URENO.

Najua vijana wa Santos watatumia muda mwingi kukaa kimya na kucheza kwenye nusu yao kwa kuwasubiri Ufaransa huku wakiwasubiri wafanye makosa na kupitia kwenye makosa yao.

UPI UBORA WA URENO…..?

Ubora wa Ureno umekuwa kwenye aina ya mchezo wanaocheza. Imekuwa timu ambayo haitabiriki kuwa kwenye mechi husika itacheza mfumo gani. Mpaka kufikia hapa tumeona Ureno nne zenye uchezaji tofauti. Santos ametengeneza timu yenye nidhamu kubwa kwanza kwa kuweza kuwafanya wachezaji wafuate anachowaelekeza, pili kwa kujilinda kwa nidhamu.

Ubora mwingine wa Ureno upo kwenye safu ya Ushambuliaji, kwani Nani na Ronaldo wamekuwa wachezaji ambao ni hatari wakifika eneo la timu pinzani. Pia Uwepo wa Renato Sanchez umeifanya timu iwe hai pindi inaposhambulia.

UDHAIFU WA URENO………………..

Aina ya umilikaji wa mpira wanaomiliki Ureno umekuwa aina isiyovutia. Timu imekosa kiungo mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na kupiga pasi nyingi ili kuifanya timu iwe na mpira kwa muda mrefu. Wamekuwa wakicheza sana kwenye nusu yao . Hii huwa ni hatari kwani inampa nafasi adui kukukaribia mara kwa mara.Udhaifu mwingine wa Ureno ni kucheza bila kushinda ndani ya dakika 90. Ni mechi moja tu waliyoshinda ndani ya dakika 90 nayo dhidi ya Wales . Pia Ureno imekuwa ikicheza Faulo nyingi sana ambazo kama Refa atakutwa si rafiki kwao inaweza kuwaletea matatizo kwa kupata kadi nyingi.

Wakifanya hivi wanaweza wakawa mabingwa wa EURO 2016.

Kwanza wasikubali kuzuia muda wote wa mchezo. Pili watumie mfumo wa 4-4-2 unaobadirika kila muda kutokana na hali ya mchezo. Kwa mfano, kwenye mechi ya leo Ni muhimu sana kwa William Carvalho kukaa mbele ya mabeki wanne, na anatakiwa apewe jukumu la kutokwenda mbali sana na eneo lake. Hii itawafanya Ureno wakati wakushambulia timu kuwa inatumia mfumo wa 4-1-3-2. Hapa timu itakuwa na Uwiano mzuri wa eneo la nyuma na mbele hivo kuwa salama hata wakishambuliwa kwa kushtukiza. Pia wakati wa kushambuliwa wawe wanabadilika kwa kucheza 4-3-1-2. Hii inaongeza nguvu ya kujilinda na itawapa nafasi nyingi za kutengeneza mashambulizi ya kushtukiza. Uzuri unapofanya mashambulizi ya kushtukiza unakuwa na nafasi ya kujilinda pindi timu inapopoteza mpira kwa bahati mbaya kwani wachezaji wengi wanakuwa hawajahama kwenye nafasi zao ila wachahe ndiyo wanakuwa kwenye harakati za kusukuma mashambulizi.
 
Nakumbuka kombe hili la Euro 2004 host country ilikuwa Ureno chini ya usimamizi wa kocha Scholari, Ureno ilipoteza ubingwa fainal baada ya kufungwa goli 1 na ugiriki, Christian Ronaldo alilia km mtoto mdogo baada ya kufanyika juhudi zote kwenye ukuta wa ugiriki ilishindikana.

Ureno ilikuwa na mashabiki wengi sana mpk 2006 kombe la dunia kutolewa ktk hatua ya nusu fainali. Kuchukua nafasi ya 4 baada ya kichapo cha Germany kupitia mashuti matatu nje ya box ya Basten Shwerztiger(mpk leo simsahau)

Niliimiss ureno ya kina Luis Figo, Deco, Maniche, Rui Costa, Sabrosa Simao, Nuno Gomez nk

#Team Ureno
 
hawa ndio wafaransa waliosababisha louis figo kuvua jersey uwanjani kabla mechi haijaisha huku zidane akiwa na mpira mkononi

nipo france
France wakilikosa kombe hili yatakuwa ni maajabu mengine ya dunia sbb uwanja wao,mashabiki wao,kila kitu kinachotumiwa na ureno chao! Halafu iweje tena! Hakuna cha ronaldo wala nini.ureno watakalishwa bila kutaka! Natabiri kuwa fainali isiyovutia.mchezo utakuwa wa upande mmoja tu
 
France wakilikosa kombe hili yatakuwa ni maajabu mengine ya dunia sbb uwanja wao,mashabiki wao,kila kitu kinachotumiwa na ureno chao! Halafu iweje tena! Hakuna cha ronaldo wala nini.ureno watakalishwa bila kutaka! Natabiri kuwa fainali isiyovutia.mchezo utakuwa wa upande mmoja tu

Sababu ulizoweka hazina mashiko.

Ureno atapigwa sababu ni kibonde kwa France ya sasa.

Allez les Bleus.
 
Sababu ulizoweka hazina mashiko.

Ureno atapigwa sababu ni kibonde kwa France ya sasa.

Allez les Bleus.
OK.hebu wewe weka sbb zako kudhihirisha huo ukibonde wa france maana mie nimejaribu weka sababu zangu
 
Nadhani hujanielewa naomba urudie tena kusoma comment yangu.

Nimekubaliana na conclusion yako ila sababu ulizoorodhesha ndiyo sikubaliani nazo.

Hata kama hii mechi ingehamishiwa uwanja WA taifa Dar Es Salaam bado France ndiyo ningeweka pesa yangu.

Kama umefuatilia toka ngazi ya makundi ya haya mashindano, utakubaliana nami kuwa Ureno hawajacheza kiwango cha kuifunga France toka mwanzo labda hii ndiyo iwe mechi ya kwanza kucheza katika kiwango hicho.

Kama umenielewa.
Poa.tupeane hi baada ya mechi kuisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom