Nina wasiwasi wa kuachana na mpenzi wangu sababu ya ugumu wa maisha na pesa

Katika maisha kitu ambocho hutakiwi kung'ang'ania ni mapenzi utakuja kujuta baadae na itakuwa ushachelewa
 
Siku ya leo nimewaza mbali kuhusu mpenzi wangu nampenda lakini pia mpenzi wangu ananipenda pia lakini hofu nilionayo tutaachana na mpenzi wangu maana sina uhakika kama kweli

1. Ataweza kuvumilia hali yangu nilionayo maana anafanya kazi ya maana mimi bado kimaisha sieleweki?

2. Nawaza je familia yao itanikubalia nimuoe mtoto wao ukiangalia mpenzi kanizidi kielimu na kimaendeleo?

3. Je ikitokea kuna mwanaume amependa na yupo vizuri kimaisha na yupo serious anataka kumuoa hali itakuwaje akiniacha nijiulaumu mwenyewe au nimlaumu yeye mwenyewe?

Naombeni ushauri wenu wadau nimewaza mbali ili nijiokoe mapema nifanye nini ili niwe na amani?
Changamsha akili huyo mwanamke anakupenda. Unadhani hakutani na wenye hela?
Tumia fursa kujenga empire yenu wewe na yeye kama una akili
 
Back
Top Bottom